SHDEPHA BUKOMBE. HUDUMA BURE KWA WAZEE BADO NI CHANGAMOTO.

Share it:










Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita ina idadi ya wazee wapatao  5704  Huduma ya  Afya kwa wazee  hao bado ni changamoto pamoja na Sera ya Serikali ya kuhakikisha wazee waliofikisha umri wa miaka 60 nakuendelea wanatibiwa bure katika hospital zote Nchini.

Hayo yalibainishwa jana kwenye kikao cha wazee na wadau wa afya ustawi wa jamii na waandishi wa habari wilayni Bukombe mkoani Geita.

Mzee Radslaus Mgalula , bibi Getruda Sizya  na Mzee Enock Bugumba  waliwaeleza wadau kuwa pamoja na jitihada za serikali kuwatambua wazee kuhusiana na huduma za matibabu bado Changamoto zinazowakabiri wazee hao ni pamoja na uhaba wa dawa, umbali wa kufikia huduma hizo.

Wamesema  zipo changamoto za vyumba vya huduma havitoshi ,wazee kutokuthaminiwa na hivyo wanamuomba mh Rais Magufuli kupitia waziri wake wa afya awatazame kwa jicho la huruma kwani bado wanateseka hospitalini hakuna dawa.

Wazee hao  walisema  wanakalishwa kwa muda mrefu kwenye foleni pia wanaomba nao waingizwe kwenye mpango wa kufuatwa na gari la wagonjwa kama mama mjamzito afatwapo huko kijijini kwani nao nguvu zimewaishia.  

Afisa ustawi wa jamii Wilayani humo,Amon Kafiriti alisema kuwa idara yake imejipanga kutoa elimu ya kuwalinda wazee ili jamii hiepukane na imani za ushirikina zinazopelekea  kuwaua wazee kwa kuwakata mapanga kwa kisingizio cha uchawi.

Aidha mganga aneyehudumia chumba maalumu cha wazee katika hospital ya wilaya  Dr Kabula Mwigulu amekili kuwa changamoto hizo kwa wazee zipo ni kutokana na ufinyu wa bajeti fedha za kununulia dawa na vifaa tiba hazitoshi  sambamba na uhaba wa miundo mbini ya majengo hayatoshi ndiyo maana sehemu nyingi wazee wanataabika.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Bukombe Nikas Safari  ametoa wito kwa wananchi kuchangia elfu 10 kila kaya ili zipatikane fedha ambazo itakuwa jawabu la changamoto zinazowakabiri wazee.

Safari alisema wananchi waliopo Bukombe wapatao laki mbili wakichangia hiyo fedha dawa ,vifaa tba miundo mbinu katika zahanati ,hasptal vitapatikana.

Hivyo aliwahamasisha waheshimiwa madiwani wakasimamamie ujenzi haraka wa zahanati kila kijiji ili kuondoa tatizo la kupata huduma mbali .

Imeandaliwa na Peter Makunga.











Share it:

habari

Post A Comment: