Wakulima wakiwa katika uwandaaji wa shamba moja kati ya mashamba yaliyopo wilayani Bukombe. |
Shamba la mboga mboga likionekana likiwa limestawi . |
GEITA:Afisa Kilimo Umwagiliaji Na Ushirika Wilaya Ya
Bukombe Mkoani Geita, Joseph Machibya
Amewataka Wakulima Wa Mazao Ya Chakula Na Biashara Kuanza Kupanda Mbegu Kwa
Kutumia Mvua Zinazoendelea Kunyesha Ili Kuendasambamba Na Msimu Wa Kilimo
Wa Mwaka 2016/17
Machibya Amesema Kwa Mujibu Wa Watabiri Wa Hali Ya Hewa,
Mvua Hizo Ni Chache Katika Ukanda Wa Ziwa Victoria Hivyo Kila Mkulima
Anapaswa Kuanza Kupanda Mazao Yake Kwa Kutumia Mvua Hizo Ili Kuenda Na Msimu
Na Kuongezeka Kwa Uzalishaji Wa Mazao .
Ameendelea Kufafanua Kuwa Wataalamu Wa Kilimo Wilayani Humo Wako Tayari
Kushirikiana Na Wakulima Katika Kutoa Elimu Ili Kuongeza Uzalishaji Wa
Mazao Ya Biashara Na Chakula Kwa Wakulima.
Kwa Upande Wake Mkuu Wa Wilaya Ya Bukombe Josephat
Maganga Amewataka Wakulima Hao Kununua Mbegu Katika Makampuni
Yaliyoteuliwa Na Serikali Ambayo Yanauza Mbegu Zenye Ubora Na Si
Kwingineko Ambazo Zitakuwa Na Ubora Na Zenye Uwezo Wa Kuota Kwa Wepesi Zaidi.
Na Makunga Peter .
Post A Comment: