Baadhi ya miti ikiwa imekatwa katika moja kati ya mistu iliyopo Wilayani Bukombe. |
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Bukombe
mkoani Geita Josephati Maganga amepiga marufuku shughuli za kibinadamu
zinazoendelea kufanyika katika msitu wa hifadhi
ya biharamulo .
Maganga amesema kuwa baada
ya kutembelea ndani ya msitu huo kwa
wiki moja kwa ushirikiano na maafisa wa wakala wa mistu nchini (TFS) wamefanikiwa kubaini uharibifu mkubwa
wa msitu huo unaochangiwa na baadhi ya watu walioingia ndani ya msitu kinyume
na sheria ya hifadhi za misitu namba 14 ya mwaka 2002.
“Hii sheria ya misitu imetoa makatazo inasema tusifanye
mambo yafuatayo la kwanza tusifanye shughuli za kibinadamu ndani ya misitu,
ulimaji unasabaibisha kukata miti, ukikata miti itaisha, malisho ya mifugo kwa
hiyo Serikali inasema hapana kuingia kwenye misitu na kukata miti” alisisitiza
Maganga.
katika hatua nyingine Maganga ameongoza kikosi cha kamati ya
ulinzi na usalama wilaya, katika kuwaondoa wavamizi wa hifadhi hiyo na
kufanikiwa kukamata zana haramu za uvunaji misitu, mifugo na kubomoa vibanda
214 vya makazi ya watu.
kwa upande wake meneja wa wakala wa hifadhi za mistu
wilayani humo (TFS) Zacharia Kitare
ameelezea katika msitu wa hifadhi ya Kahama
Biharamulo yenye jumla ya hekta mia moja thelathini na nne elfu na mianane
sitini na nne 864 wilaya ya bukombe ina miliki hekta elfu 14 pekee na
kati ya hizo hekta elfu tatu mia moja
hamsini zimekwisha haribiwa na wanachi waliovamia msitu
huo.
Imeandaliwa na Madukaoline.
Post A Comment: