Kikosi cha Buseresere kikiwa kwenye mazoezi kikijiandaa dhidi ya Timu ya Ibondo FC Kwenye ligi iliyopigwa kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Buseresere. |
Makamu mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Chato,Joseph Ng'wanzalima akisalimiana na wachezaji wa timu ya Ibondo FC. |
Wachezaji wakiendelea na mpambano. |
Mashabiki wakitazama kwa makini pambano la kati ya Buseresere Fc vs Ibondo. |
Meza kuu ni diwani wa kata ya Buseresere Godfrey Miti aliyevaa kofia ya bendera ya Taifa na Katibu wa ccm wilaya ya chato,Hamisi Kula wakiteta jambo wakati mechi hizo zikiendelea. |
Michuano ya Diwani Cup kata ya
Buseresere Wilayani Chato Mkoani Geita
ilianza tarehe 28 mwezi wa 9 mwaka huu imemalizika jana kwa
kuzikutanisha timbu mbili ambazo ni Buseresere Fc na Ibondo Fc zote zikitokea
katika kata hiyo.
Timu ya Buseresere fc imefanikiwa
kuibuka bingwa baada ya kuichapa Ibondo FC kwa jumla ya Mabao 4 kwa
1 katika fainali hiyo. iliyo iliyochezewa katika uwanja wa shule ya
sekondari Buseresere.
Timu zote mbili zilianza
kushambuliana kwa zamu kutokana na pambano hilo kutawaliwa na hofu kwa kila
timu kufungwa bao la mapema katika dakika za mwanzo za mchezo .
Katika dakika ya 31 ya mchezo
kipindi cha kwanza Ismail Adidas aliiandikia bao la kwanza timu ya Buseresere
kwa mkwaju wa penati baada ya kuchezewa madhambi na Baraka Emmanuel katika eneo la hatari bao
hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
kipindi cha pili timu ya Ibondo fc haikuwa na
maelewano mazuri katika safu ya ulinzi
ndipo mnamo dakika ya 50 ya mchezo Baraka Emmanuel akahiandikia bao la pili
Buseresere Fc na katika dakika ya 70 ya mchezo
Kanzi Majuto akaiongezea bao la tatu Buseresere Fc
Mnamo dakika za lala salama timu
ya Ibondo ilionekana kuliandama lango la timu ya Buseresere katika dakika ya 80
walifanikiwa kupata bao moja kupitia kwa mshambuliaji wao ,lakini katika dakika ya 90 ya mchezo kabla
ya muamuzi wa pambano hilo kupuliza kipenga cha mwisho Baraka Emmanuel
aliiandikia Buseresere bao la 4 na kuhitimisha kalamu ya magoli.
Hadi muamuzi wa pambano hilo
anapuliza kipenga cha mwisho Buseresere fc 4
Ibondo fc 1.
Akizungumza na madukaonline blog nahodha
wa timu ya ibondo fc Alex Method baada
ya pambano hilo kumalizika amesema kuwa
walikuwa wamejianda vizuli kwa pambano hilo lakini makosa madogomadogo
ndiyo yaliyo pelekea kupoteza mchezo huo.
Kwa upande wake nahodha wa
Buseresere fc Magesa Elikana amesema
kuwa chanzo cha ushindi huo ni juhudi zao pindi walipo kuwa uwanjani kitu
ambacho kilipelekea kushida mchezo hilo.
Kwa upande wake mgeni rasmi
katika fainali hiyo , Hamisi Kula ambae
ni katibu wa ccm wilaya ya chato amewaasa vijana wasiwe na hasira pindi wawapo
uwanjani na kuzingatia mashariti ya mchezo wa mpira.
Miongoni mwa timu 8 zilizo
shiriki ligi hiyo timu moja ya mapinduzi united
ilijikuta ikipigwa lungu la kufungiwa miaka 3 ya kutojihusisha na michezo yeyote katika kata hiyo kutoka na na utovu wa
nidhamu baada ya kumpiga muamuzi na kuzua tafrani kubwa jambo ambalo lilihatarisha
maisha ya watu katika nusu fainali ya pili ambayo walikuwa wakicheza na Buseresere
fc.
Mwandaaji wa mashindano hayo
ambae ni Diwani wa kata ya Buseresere Godfrey Miti ameelezea zawadi walizokuwa wameendaa kwa
mshindi wa kwanza ni kiasi cha sh,300,000 wapili sh,200,000 na watatu ni
sh,100,000 huku zawadi zingine zikitolewa kwa mchezo bora na mfungaji bora.
Imeandaliwa na Mrisho
Sadick,Picha na Madukaonline
Post A Comment: