Kikosi cha Yanga kwenye picha ya pamoja. |
Kikosi cha Azam FC kikiwa katika picha ya pamoja. |
Baada ya
kupokea vichapo mara tatu mfululizo timu ya Azam Fc imeambulia sare ya
bila kufungana na Mabingwa watetezi Yanga mchezo uliomalizika muda mfupi
katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Mpira ulianza kipindi cha pili na Azam walicharuka na
kufunguka zaidi na kuliandamana lango la Yanga na beki Vicent Andrew aliumia
tena na nafasi yake aliichukuwa mkongwe Canavaro.
Azam wameendelea kukosa huduma za Shomari Kapombe na
Paschal Wawa ambao bado wako na majeruhi wakati wapinzani wao wamekosa huduma
za Amis Tambwe,Haruna Niyonzima na Vicent Bossou pamoja na Malimi Busungu.
Kwa matokeo hayo Azam wamefikisha alama 12 wakati
Yanga wao wanakuwa na pointi 15 nafasi ya tatu na kwenye msimamo Vinara Simba
bado wanang’ang’ania kileleni wakiwa na pointi 23.
Uwanja wa CCM Kirumba wenyeji Toto wameendelea kugawa
pointi baada ya kutandikwa na vibonde wa Ligi jumla ya magoli 2-1 na Wenyeji
walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Yusuph Amos wakati ya Majimaji yote
yamefungwa na Peter Mapunda na kufikisha alama Sita na wakiendelea kushika
mkia.
Post A Comment: