VIJANA WAMETAKIWA KUJITUMA KWA KUJIAJIRI

Share it:
Mbunge wa jimbo la Geita Mjini Costantine  Kanyasu akiwahimiza  vijana kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kuchangamkia  fursa ambazo bado hazijafanyiwa kazi Mkoani Geita.


Baadhi wa wajumbe wa kikao hicho wakifatilia kile ambacho kilikuwa kikiendelea meza kuu.

Baadhi ya viongozi  wa chama wakiwa meza kuu.

Katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Mkoani Geita Salome Nyombi akielezea kazi zinazofanywa na umoja huo ndani ya chama.



Kutoka kulia  wa kwanza ni  Mbunge wa jimbo la mjini Constantine Kanyasu wa pili ni mbunge wa Jimbo la Geita vijijini Joseph Msukuma na anayefatia ni Innocent Kasiga Mwenyekiti wa uvccm(W)Geita.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Geita Barnabas Mapande akiteta jambo na vijana .



Mtangazaji wa kituo cha Storm fm kilichopo Mkoani Geita,Poul Bahebe akichangia mada ya namna ambavyo vijana wanaweza kuinua vipato vyao kwa kujitegemea.


Katibu wa  umoja  wa vijana wa ccm Wilayani humo Ally Rajabu amekumbushia swala la asilimia tano za vijana  

Baadhi ya vifaa ya jezi  zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Geita.


Mbunge Kanyasu akionesha mpira wa miguu.



TABIA ya vijana kutojishughulisha na kubuni miradi mbali mbali  na kutegemea shughuli ya dhahabu pamoja na miamba taka (magwangala) Mkoani Geita ni moja kati ya tabia  ambazo zimeendelea kusababisha kudorora kwa uchumi  wa Mkoa huo.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa jimbo la Geita mjini Constantine Kanyasu wakati alipokutana   katika kikao  cha umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi ccm wilayani Geita,kilichokuwa kikifanyika katika ofisi za makao makuu ya chama hicho Mkoani humo.

Alisema kumejengeka dhana kwa vijana kushindwa kujishughulisha na kufanya kazi kwa bidii na mwisho wa siku kuishia katika vijiwe vya kahawa hali ambayo imeendelea kuwazorotesha na mwisho wa siku kutambua kuwa fursa pekee Mkoani humo ni madini pekee.

“Matajiri walio wengi sio wasomi na wala hawajasoma sana lakini walichokifanya katika masiha yao ni kujituma na kutumia muda wao mwingi kubuni mambo ya msingi na ya maana katika maisha yao hatuwezi kuwa ni watu wakuilaumu serikali bila ya sisi kuwa na uthubutu”.Alisema Kanyasu.

Aidha katibu wa  umoja  wa vijana wa ccm Wilayani humo Ally Rajabu amekumbushia swala la asilimia tano za vijana  ambapo amefafanua kuwa kupitia halmashauli zilizopo Mkoani humo kumekuwepo na uzembe wa kutokutenga asilimia hizo kutoka katika  makusanyo ya ndani na hivyo vikundi  vingi vya vijana kutopata mikopo.hivyo amewataka  wakurugenzi kupitia kamati ya fedha kutenga fedha hizo ili ziendane na makusanyo yao ya ndani badala kutoa fedha kidogo.

Moja kati ya watangazaji  wa kituo cha radio Storm fm kilichopo Mkoani Geita,Poul Bahebe alipata fursa ya kuchangia mada ya vijana na uchumi ambapo amewataka vijana kuchangamkia fursa zilizopo Mkoani humo ikiwa ni pamoja na kujiajiri na kufanya kazi kwa bidii.


Pamoja na hayo mbunge Kanyasu ametoa vifaa vya michezo ambavyo vitawasaidia vijana kujiendeleza katika michezo.

Imeandaliwa na Joel Maduka
Share it:

habari

Post A Comment: