Mtuhumiwa anayedaiwa kuhusika na tukio la ubakaji kwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14 Mwalimu Bernard Lwendera akitolewa nje huku akiwa kwenye uwangalizi kwaajili ya maojiano. |
Binti aliyefanyiwa kitendo hicho akionekana kwa nyuma wakati alipokuwa akichukuliwa maelezo na afisa elimu. |
Baba wa binti aliyebakwa ,Dunia Twimanye akilalamikia jeshi la polisi kwa kumnyima ushirikiano wa kumkamata mtuhumiwa pamoja na kwamba alikuwa mitaani akizurula. |
Rehema Majaliwa ameviomba vyombo vya sheria kuchukua hatua kali kwa mwalimu huyo dhidi ya kitendo alichokifanya cha ubakaji. |
Nje ya kituo cha Polisi cha Rwamgasa. |
Mtuhumiwa akitolewa ndani ya mahabusu katika kituo cha Polisi cha Rwamgasa. |
Mtuhumiwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi baada ya kuwa ametolewa nje kwaajili ya maojiano na waandishi wa habari. |
Wananchi wakishangaa tukio hilo katika kituo kidogo cha polisi cha Rwamgasa. |
JESHI la Polisi Mkoani Geita linamshikilia mwalimu wa shule
ya msingi Mwenge katika kata ya Rwamgasa wilayani Geita Bernard Lwendera ( 29)
kwa kutuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la tano jina linaifadhiwa( 14)
ambae pia huyo mbakaji ni mjomba wa motto huyo.
Tukio hilo limetokea
usiku wa kumkia maadhimisho ya
mtoto wa kike Duniani ambapo mwanafunzi huyo alikuwa nyumbani kwa shangazi yake
kwa ajili ya kumsaidia kazi.
Akizungumza na Madukaonline blog iliofika kituo cha
polisi cha Rwamgasa mama mzazi wa mtoto huyo Rehema Majaliwa ameviomba vyombo vya sheria
kuchukua hatua kali kwa mwalimu huyo huku baba mzazi Dunia Twimanye
akilalamikia jeshi la polisi kwa kumnyima ushirikiano wa kumkamata mtuhumiwa pamoja na kwamba alikuwa
mitaani akizurula.
“Tukio hili limetokea juzi lakini nilipokwenda kuripoti
katika kituo cha polisi Rwamgasa ili wamkamate mtuhumiwa nilinyimwa ushirikiano
na mkuu wa kituo huku akinitaka nifanye mazungumzo jambo ambalo niliamua kutafuta namba ya mkuu
wa wilaya ya Geita na kumpigia na muda si mrefu alifika na kunisikiliza” .alisema
Dunia baba wa mtoto.
Naye mwanafunzi aliyebakwa ameeliza jinsi alivyofanyiwa
kitendo hicho cha kinyama na mjomba yake huku mwalimu akikana kufanya hivyo na
kudai huenda mke wake alimtegenezea mtego ili akamatwe kwani walikuwa na
ugonvi.
“Mimi nilikuwa namsadia kazi za nyumbani, na mjomba
alinituma nimtegee chakula baada ya kumaliza kumpatia chakula kabla hajanza kula alinipiga mtama (ngwala) na
kuanza kunibaka niliumia sana kutokana na kitendo hicho ndio maana nilikwenda
kumwambia mama” alisema mwanafunzi.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Geita
aliyefika kwenye tukio hilo la kusikitisha na kushangaza watu wengi ambaye ni
mkuu wa wilaya hiyo mh Hermani Kapufi amesema kwa kutumia rungu lake alilokabidhiwa
na rais Jonhn Pombe Magufuli atahakikisha sheria inachukua mkondo wake kwa
mtuhumiwa ili liwe fundisho kwa wengine.
Ofisi ya wilaya ya mkuu wa wilaya ya Geita imepokea taarifa
moja tu ya kubakwa kwa mtoto huyo huku kukidaiwa kuwa na matukio mengi yamekuwa yanatokea
lakini wahusika wakimalizana kwa kuongea na kupeana mifugo jambo ambalo
linakuwa ni vigumu kuwabaini.
Imeandaliwa na Adelina Ukugani Picha na Madukaoniline
Post A Comment: