Wananchi wakisubilia kupatiwa huduma ya macho . |
Mgeni Rasmi akitembelea baadhi ya mabanda ya kutolea Huduma . |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita,Mwandisi Modest Aporinal akizungumza na wananchi katika viwanja waliofika kupatiwa huduma ya upimaji pamoja na kufunga maadhimisho hayo. |
Wananchi wakifatilia kwa makini kile ambacho kinaendelea katika viwanja hivyo. |
Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi akihutubia wananchi katika maadhimisho ya afya ya macho. |
Mkuu wa wilaya akimtunza mcheza moja kati ya waimbaji wa nyimbo za asili wilayani Geita |
Hapa Mkuu wa wilaya akijaribu kucheza ngoma hiyo ya asili ya kabira la wasukuma. |
Huduma za upimaji zikiendelea katika vibanda vya kupimia afya na kuchangia Damu. |
GEITA:Ikiwa leo ni siku ya afya ya
macho duniani inakadiriwa kuwa takribani watu milioni 285 duniani wana matatizo
ya kuona kati yaa hao,milioni 39 wana upofu na milioni 249 wana uoni hafifu.
Hayo yamesemwa na mganga
mkuu wa mkoa wa Geita Joseph Kasala katika
maadhimisho ya siku ya afya ya
macho yaliyofanyika Kimkoa katika
halmashauri ya mji wa Geita.
Kasalama amesema asilimia 80
ya matatizo yote ya kutokuona yanayoikabili Dunia yanachangiwa na sababu zile
zinazoweza kuzuilika.Idadi kubwa ya watu wenye matatizo ya kutoona (asilimia)
wanaishi katika nchi zinazoendelea ,asilimia 82 ya watu wasioona ni wale wenye
umri wa zaidi ya miaka 50 watoto milioni 19 Duniani wanamatatizo ya kuona .
Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa
ambae ndie alikuwa ni mgeni rasmi katika shughuli hiyo mkuu wa wilaya ya
Geita,Herman kapufi,amefafanua kuwa ni
vyema kwa wananchi ambao wanatatizo la uoni hafifu kujenga destuli ya kupima
macho mala kwa mala.
“wale wote ambao tunaona wanauoni hafaifu wanatakiwa
wajitokeze kupima kwa haraka ili kunusuru macho kutokuona kabisa”Alisema Kapufi
Baadhi ya wananchi
walijitokeza katika zoezi la kupima macho wameeleza kuwa wameona ni muhimu
kuangalia hali ya afya ya macho na kwamba ni vyema kwa serikali kuendesha
kampeni hizi na maeneo ya vijijini.
Maadhimisho ya Afya ya macho
yameadhimisho mkoani na wilayani Geita,huku kauli mbiu ya siku hiyo
ikisema”afya ya macho kwa Wote ikiwa ni ujumbe mahususi kuwa umoja ni nguvu
zaidi.
Imeandaliwa na Joel Maduka
Post A Comment: