Wananchi wa kijiji cha Buyagu wakitoka katika ofisi za chama cha mapinduzi ccm walipokwenda kupeleka malalamiko yao juu ya vitendo ambavyo wamekuwa wakifanyiwa. |
Samwel Manoni ambae ni mwananchi wa kijiji cha buyagu akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya amani ilivyo kwa sasa katika kijiji chao. |
Nyumba ambayo inasadikika ya watu ambao wanajihusisha na wizi wa mifugo ikiwa imebomolewa na wananchi wenye asira kali kijijini hapo. |
Diwani wa kata ya Nyamwaga Thomasi Kayange akizungumza na wanakijiji juu ya swala la kushughulikia amani kijijini hapo na wananchi waondokane na wasi wasi wa kuvamiwa |
GEITA:Wananchi wa kijiji
cha Buyagu kata ya Nyakamwaga wilayani na Mkoani Geita wamelilalamikia jeshi la polisi ,mgambo pamoja na mwenyekiti
kijiji hicho Chayayi Michael kushirikiana na wezi wa mifugo kisha
kuwakamata wananchi na kuwatoza fedha bila kuwafikisha kwenye vyombo vya
sheria.
Malalamiko hayo yamekuja
baada ya kutokea wizi wa ng’ombe kijijini hapo uliotokea Novemba mosi mwaka huu na kusababisha vifo vya watu wawili (2)
waliouawa na wananchi wenye hasira kali,kisha kuchomwa moto ambapo kabla ya
kuuawa kwa watu hao,waliwataja Andrea Said na Mussa Lushinge kuwa wameshiriki
pamoja kwenye wizi huo.
Inadai kuwa baada ya kuchomewa nyumba moja kati ya watu
wanaoshutumiwa kuhusika na swala la wizi wa mifugo kijijini hapo anayejulikana
kwa jina la Mussa Lushinge kwa kushirikiana na wenzake walianza kuwatafuta Wananchi wanaowahisi
kuhusika na tukio hilo kwa kumshirikisha mgambo, kitendo ambacho kimelalamikiwa
na wananchi kwani pindi wanapokamatwa hutakiwa kulipa fedha na
wanapokataa hutishiwa na kubambikiwa kesi ya mauji jambo ambalo limesababisha wanaume wengi
kukimbia miji kwa madai ya kuhisi kukamatwa na kundi hilo ambalo limekuwa
likifanya msako wa mara kwa mara.
Mmoja kati ya wananchi
hao ambae anajulikana kwa jina la Samweli Manoni ameielezea madukaonline kuwa wananchi wengi wamekuwa wakikimbia na
wengine kulala madarasani na maporini kwa hofu ya kuogopa kukamatwa.
“Wananchi wetu pale
wameanza kuwa wanalala hadi madarasani
kutokana na hujuma ambayo wanafanyiwa kuwa
wamefanya mauwaji na wamebomoa nyumba za watu jambo ambalo si kweli na ikafikia hatua
mwenyekiti wa kijiji akajitoa muhanga watu wakawa wanakamatwa na wanapokamatwa
bila ya kutoa shilingi laki tano
hawaachiwi”Alisema Manoni.
Licha ya wananchi
kupeleka malalamiko hayo kwa uongozi wa kijiji lakini hawakupata ushirikiano
kufuatia baadhi ya viongozi kushirikiana na watuhumiwa kuomba fedha madukaonline
imezungumza na
Mwenyekiti wa kijiji
hicho Chayayi Michael ambapo ameelezea kuto kuhusika na tuhuma hizo na kwamba
mambo hayo yapo kisiasa.
“Kinacho zungumzwa sio
kweli mimi tarehe moja nilikamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za wizi wa ng’ombe
tarehe 10 nikawa nje nilionekana sina kesi nimefika kijijini tumefanya mkutano
wakasema diwani asimamie majukumu ya kijiji mimi nikawekwa pembeni nashindwa
kujua ni wapi nahusika na wizi ambao wananchi wamewataja”Alielezea Chayayi.
Kamanda wa Polisi Mkoani
Geita Mponjoli Mwabulambo amekiri kupokea malalamiko hayo na kwamba watafatilia
na kuchunguza juu ya tuhuma ambazo wananchi wamezielezea.
Imeandaliwa na Madukaonline.
Post A Comment: