TANZANIA YANYAKUA TUZO MBILI ZA KIMATAIFA KATIKA NYANJA YA MUZIKI WA INJILI

Share it:


Nyota wa muziki wa injili nchini mwanamama Upendo JBride zamani Upendo Kilahiro amezidi kuipeperusha vyema bendera ya mwanakondoo baada ya kunyakua tuzo mbili nchini Marekani ndani ya mwezi October 2016.

Mwanamama huyo anayejulikana kwa uhodari wa kuimba nyimbo za aina zote kutokana na uwezo 

wake wa juu wa sauti, alipendekezwa kuwania katika tuzo zinazotolewa na taasisi tofauti za injili ambapo katika tuzo za Gospel Safari Music Award zilizofanyika katika jimbo la Minnesota Marekani, amejinyakulia tuzo ya 'Recording artist of the year' akiwashinda waimbaji wengine kutoka Afrika Magharibi aliokuwa akiwania nao.

Awali wiki mbili zilizopita mwanamama huyo alishinda tuzo kupitia album yake ya 'Ficho Langu' kama 'Outstanding gospel music video' katika tuzo zijulikanazo kama 'Shabach Music Award' pia ni huko nchini Marekani. madukaonline inampongeza sana dada yetu huyu kwa kazi njema ya uinjilisti anayoifanya katika kumwinua Kristo lakini pia kuufanya muziki wa injili wa Tanzania kujulikana katika mataifa mengine.






Share it:

mastaa

Post A Comment: