Kikosi cha mpira cha polisi kikionesha kombe walilonyakua katika mashindano ya nenda kwa usalama yaliyofanyika wiki nzima.
MAADHIMISHO ya wiki ya
nenda kwa usalama barabarani Kitaifa yaliyokuwa yakifanyika Mkoani Geita
yamefungwa rasmi leo,kwa kutoa elimu kwa makundi mbalimali ya kijamii ikiwa ni
mkakati wa Jeshi la Polisi kikosi cha
Usalama barabarani Kukabiliana na ajali ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya
Watanzania kila mwaka.
Akitoa taarifa ya wiki nzima ya nenda kwa usalama barababrani mkuu
wa kikosi cha usalama barabarani taifa Mohammed Mpinga wakati wa kufunga maadhimisho
hayo yaliyofanyika katika viwanja vya kalangalala
vilivyoko mjini Geita.
Mpinga alisema makundi mbalimbali yamenufaika katika Mkoa wa
Geita wakiwemo wanafunzi wengi wa mkoa huo pamoja na jamii kwa ujumla huku
waendesha bodaboda wakipewa kipaumbele kwani wao ndio wanasababisha ajali kwa
wingi.
Awali mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Geita ambaye ni mkuu wa wilaya
ya Geita Herman Kapufi wakati wa Hotuba yake alisema ajali zinaweza kuepukika
kama watu watafuata sheria na waendesha bodaboda kuvaa kofia ngumu pamoja na
abiria wao wanapowabeba kwenda sehemu mbalimbali za mkao huo.
Katika hatua nyingine Mh Kapufi alisema watahakikisha watu wote wanafuata sheria kwa
kusoma na kuwa na leseni huku akiwaasa madereva wote wanaoingia na kutoka
katika Mkoa huo kuwa na nidhamu wakati wa kuendesha vyombo vya moto.
Baadhi ya wananchi wameomba elimu ya usalama
barabarani iendelee kutolewa kwa wananchi wote kila wakati kwani wengi wao hawana
uelewa wa kutosha.
Maadhimisho ya kitaifa ya
wiki ya nenda kwa usalama barabarani yalifunguliwa Septemba 26 na Naibu waziri wa mambo ya ndani Mhandisi Hamed Masauni katika viwanja vya
kalangalala na kufungwa leo na
mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Geita na ujumbe wa mwaka huu wa maadhimisho ya
wiki ya nenda kwa usalama unasema “hatutaki ajali tunataka kuishi salama”.
Post A Comment: