SERIKALI YAZUIA MAPATO YA SIMBA NA YANGA ‘MPAKA IPATE GHARAMA ZA UHARIBIFU

Share it:

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye,Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua na kujionea uharibifu

Kutokana na vurugu za jana za mashabiki waliohudhuria mechi hatimaye Serikali imezuia mapato ya mchezo wa Simba na Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hadi hapo itakapokata gharama za uharibifu uliotokea katika mchezo huu wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari asubuhi ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kufanya ukaguzi wa uharibifu uliofanyika.

Mashabiki wa Simba walifanya vurugu hizo baada ya Yanga kupata bao la kuongoza dakika ya 26 lililofungwa na mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo , Amissi  Tambwe baada ya kupokea pasi toka kwa Mbuyu Twite kisha kugeuka mbele ya beki wa Simba Lufunga na kuachia shuti ambalo lilimshinda mlinda mlango Vicent Angban.

Kuingia kwa goli hilo  lilizua kizaazaa, wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga huku Nahodha wa Simba Jonas Mkunde alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kutoa lugha mbovu kwa mwamuzi Sanya na kupelekea mchezo huo kusimama kwa takriban dakika saba na mashabiki wa Simba walianza vurugu na kung’oa viti na kuvirusha uwanjani.
Hata hivyo Polisi walitumia mabomu ya gesi za kutoa machozi kuwatuliza mashabiki hao na mchezo ukaendelea hadi Simba walipoweza kusawazisha katika dakika za majeruhi 89 goli likifungwa na Shiza Kichuya ambaye alitokwa na machozi kwa kuipa pointi moja timu yake.

Aidha Mh.Nnauye amesema kuwa mbali na uvunjwaji wa viti, pia mageti mawili ya kuingilia, moja la upande wa Yanga na la Simba yamevunjwa.
“Tunazuia mapato ya mechi hadi hapo tathmini itakapofanyika na kukata gharama za uharibifu uliotokea,
na ukarabati mdogo utakapokamilika Uwanja wa Uhuru, Simba na Yanga zitaruhusiwa kuendelea kutumia”alisema Nnauye.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Michezo, Alex Nkenyenge alisema kuwa zaidi ya viti 1781 vilivunjwa jana, wakati kati ya Sh. Milioni 350 na 400 zikikusanywa katika mchezo wa huo, ambao mashabiki waliingia kwa tiketi za Elektroniki.




Share it:

michezo

Post A Comment: