Eneo ambalo watu wamekuwa wakipenya kinyemera kuingia katika mgodi wa GGM,ambalo linaelezwa kuwa ni hatari kwa maisha ya wananchi ambao wamekuwa wakiingia bila ya kuwa na vibali. |
Maelekezo yakitolewa na moja kati ya wataalam katika mgodi huo mbele ya waandishi wa habari wa Mkoani Geita. |
Meneja mahusiano wa Mgodi wa GGM Tenga B Tenga akifafanua na kuonesha maeneo ambayo ni hatari kwa wananchi kuingia bila ya kuwa na kibali. |
Eneo la mgodi wa GGM Kazi zikiendelea. |
Wananchi Mkoani Geita wametakiwa kufuata kanuni na taratibu
Za Kuingia Katika Mgodi Wa Dhahabu Wa Geita
(GGM),Ili Kukabiliana Na Majanga
Ambayo Yanaweza Kujitokeza Ikiwa Ni Pamoja Na Kuingia Kwenye Mashimo Kwa
Baadhi Ya Wananchi Ambao Wamekuwa Wakiingia Kinyemela Katika Mgodi Huo.
Rai hiyo imetolewa na meneja
mahusiano wa GGM Tenga B
Tenga Wakati alipokuwa akizungumza na
mtandao wa madukaoline juu ya athari ambazo zinaweza kujitokeza endapo mtu
akiingia mgodini hapo kinyemela bila ya kufuata taratibu zilizowekwa.
Aidha Tenga,Amesema kuwa endapo mtu anaingia
mgodini pasipokuwa na mavazi maalum ba bilaya ya kuwa na mwenyeji kuna hatari ambazo zinaweza kutokea ni pamoja
na kudumbukia katika mashimo ambayo yamekwisha kuchimbwa na mwisho wa siku
kujikuta akiwa amejeruhika hivyo ni
vyema kwa mtu yoyote kuingi mgodini akiwa na kibari maalum kinachomruhusu.
Hata hivyo mtafiti wa maswala ya miamba katika Mgodi wa dhahabu
wa GGM Hatari Mjinja amefafanua madhara
yanayoweza kutokea Kutokana na miamba taka(mangwangala) ni uharibifu wa
mazingira endapo kama hayatatengwa sehemu ambayo ni maalum.
Post A Comment: