WANANCHI WANAOJICHUKULIA SHERIA MKONO WAPEWA ONYO NA JESHI LA POLISI NCHINI HATUA KALI ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.

Share it:




JESHI la Polisi  nchini linatoa onyo kali kwa wote wenye tabia ya kujichukulia sheria mkononi kuacha mara moja, kwani takwimu za makosa ya kujichukulia sheria mkononi yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi katika kipindi cha Januari hadi Agosti 2016 ni matukio 705, Katika matukio hayo yaliyoripotiwa, Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 393. 

Hayo yametolewa katika taarifa kwa waandishi wa habari na Msemaji wa Jeshi la Polisi  Makao Makuu ya Polisi, ACP Advera Bulimba jijini Dar es Salaam leo, tarifa hiyo imeeleza kuwa  kuzipuuza sheria za nchi zilizopo na wakati mwingine kuzikiuka kwa makusudi na mbaya zaidi baadhi yao kufikia hatua ya kuwaua watu wasio na hatia kwa hisia. 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mwananchi yeyote anapaswa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya mhalifu au mtu yeyote wanayemtilia mashaka katika maeneo yao.

Aidha, Jeshi la Polisi nchini, litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa kufuatilia na kuwakamata watu wote wanaojihusisha na tabia za kujichukulia sheria mkononi. 

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa watu wote wakiwemo wenye ushawishi mkubwa katika jamii kuendelea kukemea na kutoa elimu juu ya madhara ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake wananchi kuendelea kutii na kufuata sheria za nchi zilizopo.


Share it:

habari

Post A Comment: