Wilayani Geita, Mashindano ya Soka Ligi
daraja la nne (4) ngazi ya wilaya ya Geita yameanza kutimua Vumbi jana ambapo
Mechi ya Ufunguzi ilikuwa kati ya Bukoli FC dhidi ya Bomani FC na Mshindi
ameibuka Bukoli kwa goli tatu(3)didi ya Bomani kutoka mjini Geita .
Ilikiuwa siku ya jana January 19,2017 majira ya jioni ambao
Historia imeandikwa kwa mala ya kwanza baada ya miaka ishiriki ( 20)kupatikana
kwa kituo cha ufunguzi wa Ligi daraja la nne ngazi ya wilaya.
Akifungua mashindano hayo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya
Geita Mwl,Herman Kapufi ambaye alitarajia kuwa mgeni rasmi Diwani wa Kata ya
Bukoli Faraji Seif,aliwataka wachezaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika
kipindi chote cha ligi huku akiwataka mashabiki kuwa na nidhamu katika swala la
ushangiliaji.
“Natambua kuwa michezo ni ajira ni vyema kutumia nafasi hii
kwa kujituma kwa timu zote ambazo zitashiriki ligi hii na niwaombe sana wale
ambao mtashindwa mkubali kushindwa maana mchezo ni dakika sitini(90) kwa hiyo
hatutarajii kuona mnakuwa sio watu wa kuheshimiana jambo la msingi wasikilizeni
walimu wenu nikiwa na maana makocha na pia muwe watu wa kujituma kwenye mazoezi
naamini mkizingatia haya basi mtafanya vizuri timu zote”aliwasisitiza Seif
Katika mechi ya ufunguzi wenyeji Bukoli waliitandika
Boman FC mikwaju mitatu dhidi ya miwili katika kipindi cha pili .katika mchezo
huo uliochezeshwa na mwamuzi Majeshi Mgema.
Mabadiliko makubwa yalionekana katika kipindi cha pili
ambapo timu zote zilionesha ushindani na kucheza kwa kukamiana ambapo kunako
dakika ya hamsini(50) mchezaji Shukuru Mtesiga aliiandikia bao la kwanza Bukoli
FC, na dakika ya hamsini na saba (57)
mchezaji mwenzake Marius Joseph akafunga goli la pili
Bomani FC wakapata goli la kwanza katika dakika ya sitini na
saba ( 67 )kupitia kwa mchezaji wao Kasaba Sabu,na dakika ya sabini na saba
(77)kwa mara nyingine Shukuru Mutesiga aliyeonekana kinara katika mchezo huo
akaipatia ushindi timu ya Bukoli kwakuzamisha mpira kimiani na kuandika bao la tatu(3). Goli la pili la Bomani lilipatikana
kunako dakika ya themanini na mbili (82 )kupitia kwa mchezaji John Pastory.
IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE
Post A Comment: