NA EDWIN SOKO
0754551306
Naamini
kuna umuhimu mkubwa wa ushirikiano baina
ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari Nchini, nasema hivyo
kwa kuwa kama Jeshi la Polisi
litaweza kuvitumi vyema
vyombo vya habari linaweza kurahisisha
kazi zake kwa kutumia mahusiano yaliyopo baina
yake na vyombo vya habari.
Vyombo
vya habari vimekuwa na vyanzo vingi
vya taarifa na kizuri zaidi amii inaweza kuviamini zaidi
vyombo vya habari kuliko muhimili mwingine wowote, kwa misingi
hiyo hiyo wapo Waandishi wenye ujuzi wanaofanya
uchokonozi kwenye mazingira ya siri (undercover
reportage). Kwa misingi hiyo Jeshi la Polisi lilihitaji zaidi
mahusiano na vyombo vya habari kuliko uhasama.
Kitendo
kilichotokea Mkoani Geita kwa Jeshi la Polisi kuwashambulia
waandishi ni kitendo cha fedhea
kisichostahili kufumbiwa macho, dhana kuu ya
kuanzishwa kwa jeshi la polisi ni kuwalinda
raia na mali zao. Je hilo la kuwapiga
waandishi ni sahihi?
Nina
imani kwa hili la Geita kwa kuweka mbele
misingi ya utawala bora (Good Governance) Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo
awajibike na kuchukua hatua dhidi ya askari
waliohusika kuwadhalilisha na kuwapiga Waandishi Joel
Maduka wa kituo cha Radio storm Fm na Valence
Robert, mwakilishi wa kituo cha channel Ten.
Kuna
mstari wa mfananisho wa kutegemeana baina ya
Vyombo vya habari na Jeshi la Polisi, Mwanafalsafa
mmoja wa kirusi alisema kuwa, mfanano huo ni sawa na samaki na
maji.
Bila
shaka Inspector General wa Polisi Ernest
Mangu ana wajibu wa kuandaa mpango mkakati wa
kujenga maridhiano baina ya Jeshi hilo na Vyombo
vya Habari ili kuendeleza amani, kwa misingi ya
kuheshimu katiba ya Nchi na mikataba mbalimbali ya kikanda
na kidunia
Wajibu
mwingine ni kwa upande wa Vyombo vya Habari,
taasisi zake na wadau wa habari kutafuta mbadala wa
kisayansi wa kumaliza tatizo hili (scientific
possible solution) ili kuimarisha mahusiano na
Jeshi la Polisi na kuwaweka waandishi kwenye
hatua nzuri za kiusalama.
Mwisho
naamini kuwa, Jeshi la polisi na vyombo vya
habari kila mmoja ana wajibu kwenye jamii, ni kosa kwa
upande mmoja kujiona ni zaidi ya mwenzako
Post A Comment: