Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Wilaya ya Bukombe Mkoani
Geita imemfikisha mahakamani mgambo wa
kata ya uyovu, tarafa ya Siloka wilaya ya humo, Bwana IDDI KIIGE NDUMIW kwa
makosa mawili(2) ya kuomba na kupokea hongo kinyume na kifungu cha 15 cha
Sheria ya Kuzuia Na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007.
Akisomewa makosa hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Bukombe Mhe.
VERONICA SELEMAN mwendesha mashtaka wa TAKUKURU Bi. HUSNA KIBOKO aliieleza mahakama kwamba katika tarehe tofauti kati ya
tarehe 29 mwezi wa 12 mwaka jana na
tarehe 3 mwezi wa kwanza mwaka huu Mshtakiwa akiwa mgambo alimkamata Bwana
MAYUNGA NYERERE aliyekuwa amebeba magogo na kumuomba hongo ya kiasi cha
shilingi elfu kumi(10,000/=) ili asiweze kumchukulia hatua za kisheria kwa
kutoa taarifa Katika mamlaka husika.
Aidha mshitakiwa
alishawishi , kuomba na kupokea hongo ya kiasi cha shilingi elfu kumi(10,000/=)
wakati akijua kwamba ni kosa kwa mujibu wa sheria ya Kuzuia Na Kupambana na
Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007.
Baada ya kusomewa mashitaka mshtakiwa amekana mashtaka yote dhidi
yake, Mwendesha mashtaka ameiambia Mahakama kuwa uchunguzi wa tuhuma hizo
umekamilika na kuomba tarehe ambapo kesi yake itatajwa tena tarehe 18/mwezi huu
kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Geita Bw. THOBIAS NDARO ametoa shukrani
kwa raia wema wanaotoa ushirikiano kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU).
Pia Amewataka wananchi kuwa na Uthubutu na kuendelea kutoa taarifa
za vitendo vya Rushwa wakati wowote wanapohisi au kuona vinatendeka ili
watuhumiwa waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Post A Comment: