MSUKUMA AMFUNGUKIA ZITO ASEMA AMEISHIWA SERA

Share it:
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) na Mbunge wa jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku(MSUKUMA)Akizungumza na wananchi wa kata ya Nkome wakati wa ufunguzi wa kampeni za udiwani katika kata hiyo.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) na Mbunge wa jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku(MSUKUMA) pamoja na mgombea udiwani wa kata ya Nkome kwa tiketi ya chama hicho ,Masumbuko Sembe wakiingia kwenye viwanja vya mkutano

Katibu Mwenezi wa chama wilaya ya Geita ,Jonathan Masele akinogesha Mkutano huo wa hadhara 

Msukuma akisakata Lumba kwenye mkutano huo.

Mbunge wa Geita Mjini ,Constatine Kanyasu akiserebuka katika uzinduzi wa kampeni.






Mwenyekiti wa halmashauri ya mji na Diwani wa kata ya Bomba mbili ,Leornad Bugomola akizungumza katika mkutano huo.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Dotto Biteko akitoa maelezo juu ya uchaguzi mdogo unaotarajia kufanyika.


Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Geita,Barnabas Mapande akisisitiza wananchi kumchagua diwani anayetokana na chama hicho.

Mgombea udiwani katika kata ya Nkome,Masumbuko Sembe akiomba kura kwa wananchi.

Mwenyekiti Msukuma akimkabidhi ilani ya chama hicho mgombea udiwani.





Aliyewai kuwa mgombea ubunge wa  jimbo la Nyang'wale mwaka 2015 George Joseph akirudisha kadi ya chadema na kuamua kujiunga na ccm katika Mkutano huo.




Kampeni za uchaguzi mdogo kwa ngazi ya udiwani kwenye kata ya Nkome wilaya na Mkoa wa Geita,zimeendelea kupamba moto huku kila chama kikiendelea kunadi sera zake na wagombea wake kwa nyakati tofauti.
Wiki iliyomalizika siku ya jumamosi chama cha mapinduzi (CCM)kilizindua kampeni zake kwenye kata hiyo huku mwenyekiti wa chama Hicho na Mbunge wa Geita vijijini Joseph Kasheku(MSUKUMA)Akijibu juu ya tuhuma ambazo zilielezwa na Mwenyekiti wa  chama cha ACT wazalendo na mbunge wa Kigoma kijijini Zito Kabwe kuwa ni vyema hakataja pesa za jimbo zimekwenda wapi na kwamba hajawai kusoma matumizi ya fedha hizo huku akiliomba jeshi la polisi kumkamata kutokana na kutoa rushwa ya mabasi.

Akielezea tuhuma hizo msukuma amesema kuwa pesa za jimbo hazina siri kwani alipoingia kwenye kiti cha ubunge mwaka jana jumla ya kiasi cha sh,milioni  thelasini na tisa(39) katika jimbo lake ambapo pesa hizo zilifanya kazi za kutengeneza barabara pamoja na kukarabati stendi.

“Mimi ni mbunge mwaka mmoja barabara zinaonekana na nataka kuwaambia kuwa pesa za jimbo hazina siri kwani wajumbe wake ni madiwani wanne na mimi ndio mwenyekiti nataka nisema matumizi na ndio wajibu wangu kilomita sita najua kuna watu ni wanafanya kazi ya ukandarasi hapa inaghalimu kiasi cha milioni arobaini na tano(45)nimelima  Bwea kilomita nane mitambo yangu imelima nimelima barabara ya Buligi najua mimi ni tofauti na wa kwao sikwenda Bungeni kutafuta pesa za posho kama yeye Zito anavyofanya ni vyema tukazungumza maneno ya kuwakonga wananchi wetu sio kutoa poroporoganda zisizo na maana”alisema Msukuma

Msukuma aligusia pia swala na kauli yake  ambayo alitoa Bungeni juu ya kuruhusiwa kwa kilimo cha bangi .

“Ndugu zangu wanankome naomba ninukuu maneno niliyoyasema Mh,Spika katika kukuza uchumi wa Tanzania Kwasababu ya wataalam tulionao wanatudanganya  wanaenda wanachukua utaalam na vitabu vya uingereza na marekani ndio maana sina uhakika kama mirungi inashida tumeona nchi kama Kenya inaendelea kukuza kipato chake kwa kuruhusu mirungi hata Bangi sina uhakika kama inafaa kuzuiliwa ni madaktari gani ambao wamefanya uchunguzi wakabaini kuwa bangi inamatatizo je kati ya bangi na viroba vipi vyenyematatizo nilimwambie spika kuwa hata humu Bungeni kuna wabunge wanakula bagi na nilitaka kuwataja na nilizungumza kule kwetu husukumani mtu akila bangi analima hekali mbili leo mvuvi anakula bagi anakamatwa”Alisema Msukuma.

Ameendelea kusisitiza kuwa ni vyema kwa Mh,Rais Kuendelea kukaza kamba ili wale ambao walikuwa wamezoea kufisadi pesa za serikali waendelee kukiona cha Moto.


Kampeni za uchaguzi mdogo zinatokana na kifo cha aliyekuwa Diwani wa kata Michael Denja alifariki mwaka jana.



Share it:

habari

Post A Comment: