Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita,Mponjoli Mwabulambo akikanusha taarifa ya kukamatwa kwa ,Waziri mkuu mstaafu ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu Taifa ya chama cha demokrasia na Maendeleo chadema Edward Lowasa.
Waziri mkuu mstaafu
ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu Taifa ya chama cha demokrasia na Maendeleo
chadema Edward Lowassa, pamoja na ujumbe
aliokuwa amefatana nao wameshikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Geita
kwa maojiano ambayo yamedumua kwa zaidi ya masaa matatu,wakati akitokea Mkoani
Kagera ambapo alifika kwenye stendi ya mabasi ya zamani kwa lengo la kusalimiana na wananchi wakati akipita
kuelekea kwenye kampeni za uchaguzi mdogo kata ya Nkome.
Tukio la kukamatwa kwa
waziri mkuu huyo,lililoambatana na vipigo vikali kwa waandishi wa habari
wawili,Valence Robert wa Chanel Ten na Joeli Maduka wa Storm Fm ambaye pia ni
mmiriki wa mtandao wa madukaonline blog ya mjini Getia limetokea leo majira ya saa
9:30 jioni eneo la stendi ya zamani ya mabasi iliyopo katika kata ya
kalangalala mjini Geita.
Lowassa ambaye alikuwa
wenye gari yenye namba T 771 DEA aina ya
V8 Land curuser na wenzake ambao ni Hamis Mgeja pamoja na Profesa Balegu
walikuwa wakitokea mjini Bukoba kuelekea mjini Geita kwenye kampeni za uchaguzi
mdogo wa udiwani unaofanyika katika kata ya nkome wilaya ya Geita Vijijini.
Kwa mjibu wa mwandishi Joel
Maduka chanzo cha Lowassa kukamatwa kilitokana na na yeye kusimama kisha
kuzungumza na wananchi waliokuwa wamekusanyika katika standi hiyo kumweleza
changamoto zinazowakabili ikiwemo ugumu wa maisha na ukame kukithiri hali
ambayo imesabauisha baadhi ya maeneo kukumbwa na njaa.
Hata hivyo saa chache
kabla ya Lowassa kujibu kilio cha wananchi hao,kamanda wa polisi wilaya ya
Geita(OCD)Ally Kitumbo alifika eneo hilo akiwa ameongozana na askari zaidi ya
kumi waliokuwa na silaha za moto kisha kumwamuru Lowassa kwenda kituo cha
polisi bila shuruti.
Kutokana na hali hiyo
baadhi ya wananchi waliamua kuandamana wakifuatilia kwa nyuma msafara wa waziri
mkuu huyo mstaafu hadi kituo kikuu cha polisi wilaya ambako yalianza
kufyatuliwa mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi ambao kwa wakati huo
walikwishaanza kujazana nje ya kituo hicho kufuatilia kukamatwa kwake.
Wakiwa kituoni hapo,na
baada ya kuhakikisha wananchi wamekimbia kuokoa maisha yao baadaye msafara wa
waziri mkuu huyo mstaafu aliyekuwa ameongozana na Profesa Balegu,na Hamis Mgeja
uliondoka kituoni hapo kuelekea makao makuu ya polisi mkoa wa Geita ukiwa chini
ya ulinzi mkali wa polisi ambako hadi mtandao wa madukaonline unakwenda
mitamboni bado viongozi hao wa chadema walikuwa ndani ya ofisi ya kamanda wa
polisi mkoa wa Geita wanakohojiwa.
Hata hivyo mbali na
polisi kurusha mabomu ya machozi na kupiga risasi za moto kuwatawanya wananchi
hao,waandishi wa habari wawili Robert na Maduka waliokuwa eneo hilo
wakitekeleza majukumu yao ya kazi walikamatwa kisha kuanza kushushiwa kipigo na
polisi huku Maduka akiumizwa sehemu za mgongoni wakati Robert akipigwa kwa
mateke sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani,mgongoni na miguuni.
Maduka na Robert
waliokolewa na OCD Kitumbo aliyefika eneo ambalo walikuwa wakipokea kipigo
kisha kuwazuia askari wake wasiendelee kuwashambulia waandishi hao ambao kwa
wakati huo walikwishakamatwa Tanganyika jeki wakilazimishwa kuingia kituoni ili
wawekwe mahabusu.
Wakizungumza na madukaonline
,waandishi hao walidai kuwa kitendo walichofanyiwa na polisi hao ni cha kinyama
na hakikubaliki kwa vile kinavunja haki za binadamu ikizingatia kuwa walikuwa
wakitekeleza majukumu yao bila kuvunja sheria za nchi.
‘’Kwa kweli nimeumizwa sana sehemu za mgongoni lakini pia
kitendea kazi changu ambayo ni Kamera ilirushwa kwa minajili ya kuivunja lakini
kutokana na ugumu wa kifaa changu hakikuweza kudhurika sasa najiuliza hivi hii
ni haki na je Tanzania kuna uhuru wa vyombo vya habari maana kama mwandishi
anavamiwa eneo lake la kazi kisha kupigwa bila sababu’’alisema Maduka.
Kwa upande wake Robert
ambaye kwa sasa anachechemea kutokana na maumivu aliyoyapata kutokana na
kipigop hicho alidai amesikitishwa na kitendo cha polisi kuvunja kamera yake
ambayo amekuwa akiitumia kutekeleza majukumu yake na hajui iwapo jeshi hilo
litamlipa au la.
Kwa mjibu wa waandishi
hao wamedai wamepanga kuchukua PF3 kisha kufungua kesi mahakamani ili kudai haki
zao kutokana na kitendo cha udhalilishaji walichofanyiwa.
Aidha klabu ya waandishi
wa habari mkoa wa Geita(GPC)mbali na kulaani kitendo hicho imeelekeza kwa
waandishi waliokumbwa na madhila hayo kuhakikisha wanapata PF3 ili baadaye
uongozi wa GPC umwandae wakili wake ambaye atasimamia kesi hiyo mahakamani.
‘’Nimesikitishwa na kitendo walichofanyiwa waandishi hao na
nimeelekeza wahakikishe wanachukua PF3 ya matibabu ili tumwandae wakili wetu
ambaye atasimamia kesi hiyo itakapofikishwa mahakamani lengo ni kuonyesha
kukerwa na vitendo vya polisi vya kuwakamata na kuwapiga waandishi bila sababu
wanapotekeleza wajibu wao wa kihabari’’alisema Mwenyekiti wa GPC Mkoa wa Geita
Daniel Limbe.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Geita Mponjili Mwabulambo amekanusha
taarifa ya kukamatwa na kwamba walimzuhia kwaajili ya usalama na maswala mengi
ambayo wamezungumzia ni jambo la ulinzi na kwamba walilenga katika swala la
ulinzi wa jamii na usalama wa wao wenyewe.
“Kiswahili
kizuri kwamba tulikuwa tumemzuhia hatukuwa tumemkatamata isipokuwa tulikuwa tumemzuia ule msafara wake
kwa ujumla nyuma ya kumzuhia kwake lilikuwa ni swala la usalama na ulinzi kwa
ujumla”alisema mwabulambo
|
Post A Comment: