Zikiwa ni siku chache tangu
mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na maendeleo chadema
Mkoani Geita Upendo Peneza kufanya mkutano
wa hadhara na Wananchi wa kata ya Kasamwa na kumwomba kushughulikia kero
ya upatikanaji wa maji katika Bwawa la kasamwa hali hii imemlazimu Naibu waziri wa ofisi ya Rais tawala za Mikoa
na Serikali za mitaa TAMISEMI Bw.Suleiman Jafo kufika na kujionea ukarabati
ulivyofanyika wa Bwawa hilo.
Katika hali isiyo ya
kawaida wananchi wa Katoro wamegoma kukubaliana na taarifa ya Utekelezaji wa
mradi wa Bwawa la Maji unaotajwa kutekelezwa kwa kiasi cha fedha Shilingi
milioni 74 kwani fedha iliyotumika ni tofauti na ujenzi wa Bwalo hilo ulivyo
kwasasa.
Hali hiyo imemlazimu
Naibu waziri wa ofisi ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI .Suleiman
Jafo aliyekuwa katika ziara ya siku moja wilayani Geita kuahidi kuunda Tume ya
Uchaguzi itakayo toa taarifa kamili ndani ya wiki tatu
“Nitaunda tume maalum ya
kuja kuchunguza mradi huu na kama fedha ambazo zimetolewa hazijafanywa kama
inavyotakiwa tutawachukulia hatua za kisheria wale wote ambao wameusika katika
ujenzi wa Bwawa hilo”alisema Jafo
Awali katika taarifa
iliyotolewa na Mhandisi wa maji wa halmashauri ya Mji wa Geita Gaspar
Shoo,imesema kuwa Mradi wa Bwawa unaohudumia wananchi wa kata za Kanyara na
Kasamwa uligharimu Milioni 74
Ujio wa naibu waziri
uliokuwa na agenda moja ya kuangalia changamoto za maji Mkoani Geita umekuja
ikiwa ni sikuchache baada ya Mbunge wa viti Maalum mkoani humo Kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Bi.Upendo Peneza kumtaka kufika kuzungumza na
wananchi na kutafuta suluhu ya tatizo
“Mimi kama Mbunge kazi yangu ni kuendelea kusema na kuwaelezea
kero zenu Bungeni na kutokana na hali hii niwaakikishie sitachoka kufikisha
kilio chenu cha uhaba wa maji kwa waziri mwenye dhamana na nitaakikisha waziri
anafika kujionea wizi uliofanyika katika ujenzi wa Bwalo hili”Alisisitiza
Upendo
IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE
Post A Comment: