Diwani wa Kata ya Nyang'oko Elias Ngolle akimwelezea Mkuu wa Mkoa changamoto ambazo zipo kwenye kata yake.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali
Mstaafu Ezekiel Kyunga amefanya ziara ya
kutembelea vijiji na mitaa katika wilaya ya Geita lengo likiwa ni kuzungumza
na kujua wananchi ambao wanapatiwa fedha kutoka kwenye mpango wa
kunusuru kaya masikini awamu ya tatu (TASAF ) wanavyofaidika na fedha hizo na namna ambavyo wamezifanyia kazi na uelewa wa
mfuko huo.
Kyunga ametembelea kwenye Kata
za Busanda,Nyakamwaga ,Nyan’goko ,Mtakuja na
Bumwongoko kubwa akikisitiza wananchi ambao wanapatia fedha hizo kutoka kwenye
mfuko wa huo kutumia kwa maendeleo ambayo yatawasaidia hata baada ya
kuwa muda umemalizika wa kupatiwa ruzuku.
“Mpango
wa kuhudumia kaya masikini ni wa miaka mitatu hadi sasa wamelipwa awamu
kumi hivyo wamebakiza awamu nane za kulipwa hivyo nawaomba wananchi kuakikisha
muda uliobaki mnatumia fedha kwa manufaa na kwa Faida zaidi ikiwa ni
pamoja na kununua vitu ambavyo vitawasaidiam kuongeza kipato kwenye familia
zenu”Alisema Kyunga.
Hata hivyo baadhi ya
wanufaika wa mradi huo wamesema kuwa tangu kuanzishwa wamefaidika na vitu vingi ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa nyumba pamoja na kusomesha
watoto hivyo kutokana na hatua hiyo wameishukuru serikali kwan maana
imeweza kuwasaidia wale ambao walikuwa awana uwezo.
“Mimi naitwa Valentino Sweya
naishukuru sana serikali kwa kuleta mradi huu kwakweli
mimi nimenufaika sana kwani nimeweza kujenga nyumba ya chumba kimoja
na sebule ,pia nimekuwa nikinunua chakula na pia nimeweza kununua nguo
za wanafunzi kiukweli nimenufaika sana na Tasaf”Alisema Sweya.
“Hatujawai
kukutana na changamoto yoyote kwenye malipo kwani tumekuwa tukipatiwa
fedha kwa msingi mzuri tatizo baadhi yetu awana elimu kabisa ya matumizi
ya fedha hizi kwani wamekuwa wakitumia pasipokujua matumizi sahihi
ya fedha hizi mimi niombe basi serikali itoe elimu ya kutosha kwa walengwa”alisema Mzee Danile Safari.
Hata hivyo katika ziara yake ya siku
Mbili kwa halmashauri zote mbili za wilayani GEITA Mkuu wa mkoa wa Geita
, amekutana na changamoto ya wanufaika wa
mradi huo kutokujua kikomo cha kupokea fedha na wengine kushindwa kutimiza
makusudio ya fedha hizo kama ambavyo zimepangwa kufanya shughuli za
kimaendeleo na kunusuru kaya ambazo hazina uwezo wa kifedha na kipato na wale,
ambao walishindwa kuwasomesha watoto.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
|
Post A Comment: