Waziri wa nishati
na madini ,Professa Sospeter Muhongo,amemwagiza Kamishina wa madini kanda ya
ziwa kutembelea migodi yote na kuikagua ili kujua hali ilivyo na kuakikisha
wanatoa mashariti katika migodi yote mikubwa,ya kati na midogo.
Hayo ameyasema wakati alipowatembelea wachimbaji kumi na tano ambao
walifukiwa na kifusi kwenye mgodi wa RZ union uliopo kwenye kijiji cha mawemeru
Kata ya Nyarugusu wilaya na Mkoa wa Geita.
Prof,Muhongo
amemwagiza kamishina wa madini kuakikisha anafanya ukaguzi na kutembelea migodi
yote na kwamba kufikia tarehe 16 ya mwezi wa tatu awe ametoa taarifa ya hali
ilivyo kwenye migodi ambayo hatakuwa ametembelea.
“Kamishina
nimekwisha waelekeza tembeleeni Migodi yote mkague na kwasababu watu
wanaendelea kuchimba kama nyie ni wachache tuongezeni nguvu kutoka
wizarani,kutoka stamiko,siorojiko au chuo kikuu leo ni tarehe 17 hadi kufikia
16 mwezi ujao nipewe ripoti ya ukaguzi”Alisisitiza Prof Muhongo.
Kamishina Msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria magharibi Yahaya
Samamba ,amemweleza waziri wa nishati na madini sababu zilizopelekea kuanguka
ni kutokana na kuzidiwa kwa udongo uliokuwa juu pamoja na kuwa ni mgodi wa muda
mrefu hivyo timba zilikuwa zimekwisha anza kuoza na kwamba hatua ambazo
zimechukuliwa hadi sasa ni mgodi kufungwa hadi yale maelekezo waliyopatiwa
yatakapo kuwa yamekamilika.
“Uchunguzi
uliofanyika umeonyesha kuwa mgodi huu umeanguka kutokana na kuzidiwa na udongo laini juu pia mwamba laini ulioza
kiasi cha takribani mita 15 kutoka usawa wa ardhi lakini pia sambamba na hilo
mgodi huu una muda mrefu zaidi ya miaka mitatu kwa hiyo zile sapoti kwa maana
ya timba zilikuwa zimekwisha hanza kuoza na tulikuwa tumekwisha wapo maelekezo
wakati wakiwa kwenye marekebisho ya kuweka chuma ndio ajali hii iliweza kutokea
kazi inayoendelea hivi sasa ni kutoa maji kwenye shimo ili kuakikisha mazingira
yanakuwa mazuri ili kufanya yale ambayo yameagizwa na kamishina wa
madini”Alisema Samamba.
Kwa upande
wake msemaji wa mgodi huo na mwanasheria,Francis Kiganga ,amemwomba Waziri wa
nishati na madini kutia sahini ya hati ya uhamishaji miliki kwa maana pande
zote mbili wamekubaliana kwa muuzaji abaki na asilimia 15 na mnunuzi ahamishiwe
asilimia 85.
Hata hivyo
ombi hilo alikukubaliwa na waziri wa nishati na madini hadi pale mgodi huo
utakapokuwa umetimiza mashariti ambayo wamepatiwa.
Hata hivyo
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi,amemweleza waziri Muhongo kuwa wamefatilia kuakikisha vijana wanapatiwa mikataba
ya kudumu .
Akizungumza
kwa niaba ya wachimbaji wenzake ambao walinusurika kwenye ajali hiyo Ansenti
Masanja amemshukuru waziri Muhongo kwa kuwatembelea na kuja kuwajulia hali zao
ikiwa ni pamoja na kuwapa pole.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: