Mwenyekiti
wa Chama Cha Wakandarasi Tanzania, Mhandisi Lawrence Mwakyambiki akisistiza
jambo kwa waandishi wahabari (hawapo pichani) mapema hii leo jijini Dar es
Salaam kuhusu Serikali kuwapa
kipaumbele wakandarasi wa ndani katika miradi ya ujenzi.
Na Eliphace Marwa, Dar es salaam
Chama cha Wakandarasi Tanzania kimeiomba Serikali kuwashirikisha katika
zabuni za ujenzi wa miradi mbalimbali ya umma Wakandarasi wazawa.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Chama hicho, Mhandisi
Lawrence Mwakyambiki wakati mkutano na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji
wa mipango mbalimbali ya Serikali katika
sekta ya ujenzi hapa nchini.
Alisema kuwa wanaiomba Serikali ya Awamu ya Tano kuwashirikisha
wakandarasi wa kitanzania , wakimemo wakandarasi wa madaraja yote ili waweze
kujijengea kitaalamu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo
ujenzi wa majengo mbalimbali ya Serikali mkoani Dodoma.
Mhandisi Mwakyambiki aliongeza kua hatua hiyo itasaidia kuongeza
ajira kwa vijana na Kampuni za kitanzania katika shughuli za ujenzi hapa
nchini.
Aidha, Chama hiyo kimeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa
mstari wa mbele katika kutekeleza mikakati na kusimamia sekta ya ujenzi hapa
nchini.
Aidha Mwakyambiki aliongeza kuwa kutokana na uamuzi wa Serikali ya
Awamu ya Tano kuhamia Dodoma ni vema wakandarasi wa ndani wakapewa fursa ya
kushiriki katika kandarasi mbalimbali ambazo serikali inatarajia kuzifanya huko
Dodoma.
Kwa upande Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam
Mhandisi John Bura alimshukuru Rais Magufuli na Serikali yake kwa kuitikia wito
wa wakandarasi kwa kuwatengea miradi michache ambayo ilikwisha tangazwa.
Aliwataka wakandarasi kuunda umoja kwa ajili ya kuitekeleza kwa
weledi ili kuongeza imani kwa Serikali.
|
Post A Comment: