Baadhi ya wana kijiji wakiwa kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Nyabalasana Kata ya kakubilo kilichopo katika halmashauri ya Wilaya ya Geita, Jimbo la Geita Vijijini wakielezea . |
Kaimu afisa mtendaji wa kijiji cha Freda Bosha akisoma taarifa ya kijiji hicho mbele ya mkuu wa wilaya ya Geita,mwalim Herman Kapufi |
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wakifatilia Mkutano huo. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara. |
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Geita, Joachim Ruweta akajibu maombi ya wananchi juu ya kupatiwa kwa umeme wa REA awamu ya pili. |
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Geita, Joachim Ruweta akiendelea kufafanua zaidi mbele ya wananchi. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herma Kapufi akikagua daraja ambalo limekuwa likisababisha wanafunzi kushindwa kupita kuelekea shuleni pindi mvua zinaponyesha. |
Moja kati ya wakazi wa kijiji hicho akiuliza swali kwa Mkuu wa wilaya ya Geita. |
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara Mahingu Masatu
na Elias Nzobe wakazi wa kijiji hicho wametoa kero yao mbele ya Mkuu wa wilaya ya Geita ambapo wamemweleza kwamba kukosekana kwa
mtendaji huyo ngazi ya kijiji imepelekea mapato mengi kupotea huku michango
wanayochanga ikiwa haieleweki inafanya kazi gani na inakwenda wapi.
“ Kero ambayo imesababisha wananchi kugoma kuchangia
madawati moja ni kutokana na watendaji wambao walikuwa wanakuja wanakusanya
michango wanaondoka sasa tutaendelea paka lini unachanga kitu akifanyiki sisi
tukaona ni bora kugoma”Alisema Maningu
“Kiini ni kutokana na swala la ujenzi wa choo
kutokukamilika wa shule ya msingi Nyabalasana baada ya wananchi kuchanga na
kuona kuwa kazi ijafanyika inavyotakiwa ndio sababu ambayo imetupelekea
kugoma”alisema Nzobe
Akisoma taarifa ya kijiji hicho Kaimu Afisa mtendaji wa kijiji hicho Freda Bosha
amebainisha namna ambavyo
mapungufu yalivyo kutokana na kukosekana kwa afisa mtndaji huku akimwomba mkuu
wa wilaya kupatikana kwa mtendaji kijiji hapo.
“Kukosekana kwa afisa mtendaji ni chanzo kikubwa cha
mapato mengi kupotea bila ya utaratibu Mh,Mkuu wa wilaya tunaomba kupatiwa
mtendaji katika kijiji ili aweze kusimamia shughuli za maendeleo kijijini
hapa”alisema Bosha
Kufuatia hali hiyo iliyochangia hata uwajibikaji wa
wananchi kuchangia upande wa Madawati kusuasua, Mkuu wa Wilaya Mwl. Herman
Kapufi pamoja na kuwahimiza wakazi wa
Nyabalasana kuendelea kujitolea katika miradi ya maendeleo
amewahakikishia kwa muda wa wiki mbili watampata afisa mtendaji, huku
akimwachia jukumu hilo Afisa utumishi.
“Lakini msiwe na tabia ya kuzira kwasababu ya mtu
furani kama kuna tatizo mnakaa kwenye kikao
mnajadili mnatafuta mwafaka mwenyekiti inaonekana kuwa amezidiwa
kutokana na kwamba akuna mtendaji wa kijiji
maana mtendandaji wa kijiji ndie mshauri bahati nzuri afisa utumishi
yupo hapa naamini hatalifanyia kazi kwani ndie mwenye uwezo wa kuhamisha
mtumishi”Alisema Kapufi
Katika hatua nyingine wakazi hao wakaliomba Shirika la
Umeme Tanzania {TANESCO} Mkoa wa Geita
kupitia mradi wa Umeme Vijijini REA
kuwafikishia nishati hiyo.
“Wananchi wanatakiwa kuchangia kwa kuachia maeneo yao
wazi ili waweze kusababisha huduma kufika kwenye maeneo ya makazi yao tunaendelea
na jitihada za kusambaza umeme kwa awamu ya pili maeneo ambayo bado umeme
ujafika”Alisema Ruweta
Post A Comment: