|
Balozi wa Jamhuri ya
Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi (katikati)
akishirikiana na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bw. Petro Ryatuu kukata utepe kuashiria uzinduzi wa maadhimisho ya wiki
ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya
Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam
|
|
Balozi wa Jamhuri ya
Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi (kushoto) akiweka
sahihi katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la maonyesho la Bodi ya
Filamu Tanzania wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa
Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo
Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu
|
|
Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu (wapili kushoto)
akiangalia moja ya kitabu kilichofanyiwa marekebisho na wataalamu kutoka Iran
baada ya kuchakaa wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa
Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo
Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji BASATA Bw. Godfrey Mngereza
|
|
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu (Wanne kulia) akiangalia bidhaa za
kiutamaduni za Iran zinazotengenezwa na malighafi za shaba, fedha na dhaabu
kutoka kwa Bw. Anmad Hamidi (kulia) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki
ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya
Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni Balozi wa Jamhuri ya
Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi |
|
Kikundi cha kiutamaduni kutoka Iran kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho
ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na
Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.
|
|
Kikundi cha ngoma kiitwacho Jivunie Tanzania
Sanaa Group kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni
wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo
Jijini Dar es Salaam. |
|
Baadhi ya washiriki wa maonyesho ya maadhimisho
ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi wakifuatilia matukio yaliyokua yakiendelea
katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es
Salaam |
|
Watoto wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran
wakiimba wimbo wa taifa wa Iran wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya
Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya
Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam. |
|
Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu (katikati)
akifuatilia maonyesho yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa maadhimisho
ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na
Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya
Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi na kulia ni
Mkurugnzi Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw. Achiles Bufure
|
|
Balozi wa Jamhuri ya
Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi (kulia)
akizungumza na watu walioshiriki katika maonyesho ya maadhimisho ya wiki ya
Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya
Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.
Picha
na:
Genofeva Matemu – WHUSM
|
Wadau wa
utamaduni nchini wametakiwa kutumia maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa
Washirazi kuenzi, kuendeleza na kudumisha ushirikiano wa kiutamaduni katika
tasnia ya Lugha, Sanaa, Filamu, Mila na Desturi za Tanzania na Iran.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Bw. Petro Ryatuu wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa
Washirazi leo Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na
Nyumba ya Utamaduni.
“Uhusiano
uliopo kati ya Tanzania na Iran ulianza tangu karne ya 18 kipindi cha majilio
ya wahenga wa kishirazi kutoka uajemi ulioacha turathi za kiutamaduni za pande
zote mbili” amesema Bw. Ryatuu.
Aidha, Bw.
Ryatuu ameushukuru uongozi na watumishi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya
Utamaduni katika kufanikisha sherehe hii adhimu ya wiki ya utamaduni wa
Washirazi.
Kwa upande
wake Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa
Far’hanqi ameushukuru uongozi wa Tanzania kuendeleza na kuthamini utamaduni wa
washirazi unaounganisha nchi ya Iran na Tanzania.
Washirazi
walikuja nchini tangu karne ya 18 kufanya biashara katika Pwani ya Bahari ya
Hindi na mji wao wa kwanza kufika ulikua ni Kilwa mji ambao uliweza kustawi
kiuchumi na kuweza kujitengenezea fedha zake yenyewe na kufanya biashara na
miji yote ya Pwani ya Afrika Mashariki.
Post A Comment: