Hakuna mtu ambaye aliweza kuamini kuwa Mabingwa watetezi wa Uhispania timu ya Barcelona itafanya maajabu katika mchezo wao dhidi ya PSG katika Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa kuwang’oa kwa 6-1 na kutinga hatua ya robo fainali.
Katika mechi ya kwanza jijini Paris, ililala kwa mabao 4-0 na kila mmoja akaamini, safari imewakuta.
Leo wameonyesha wao ni miamba ya soka licha ya bao la Edinson Cavani ambalo lilionyesha kuwa ugumu uko kwao.
Lakini Barcelona waliianza shughuli mapemaa kupitia Suarez, PSG wakajifunga kupitia Lavyn Kurzawa na mapumziko ikawa 2-0.
Kipindi cha pili, dakika ya 50, Lionel Messi akaifungia Barcelona bao la tatu lakini Cavani akafunga moja la kufutia machozi dakika ya 62.
Bao la Cavani likafanya ionekane kama shughuli imeisha kwa kuwa bao tatu zilitakiwa na Barcelona wakazitendea haki.
Neymar alianza dakika ya 88, akafunga bao la nne, akafunga la tano tena dakika ya 90 na kutoa pasi ya la sita dakika za nyongeza ambalo lilishindiliwa wavuni na Sergi Roberto. Kweli Barca si watu wa mchezo.

Post A Comment: