Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine
Mahiga (Mb.) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe.
Antonio Guterres (kushoto) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar Es Salaam jana. Mhe. Guterres alisimama kwa muda katika uwanja huo akitokea nchini Kenyakwa ajili ya kufanya mazunguzmo na Balozi Mahiga. Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Mhe Guterres aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa
juhudi zake za kutafuta amani nchini Burundi kupitia kwa Msuluhishi wa
Mgogoro huo Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Benjamin Willium Mkapa. Aidha, Dkt. Mahiga aliwasilisha Salamu Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri Mahiga akizungumza jambo huku Mhe. Guterres akimsikiliza kwa makini.
Dkt. Mahiga akiendelea kuzungumza na Mhe. Guterres huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakiwasikiliza kwa makini.
Picha ya pamoja
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,Bi. Mindi Kasiga naye akiagana na Mhe. Guterres
Mhe. Guterres akiagana na Dkt. Mahiga mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo yao.
Post A Comment: