DC KAPUFI AWAHIMIZA MAAFISA KILIMO KUTOKUKAA OFISINI NA BADALA YAKE WAFANYE UTAFITI WA MAENEO YA KILIMO

Share it:
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Katandalo kata ya Kaseme juu ya kuhimiza kilimo ambacho kinastahili ukame wakati wa Ziara ya kutembelea mashamba ya pamba mtama na Mihogo.

Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwasili kwenye ofisi za Kijiji cha Katandalo.hapa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa kijiji hicho.


Mkuu wa wilaya akisaini kwenye kitabu cha wageni Kijiji cha Katandalo.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwasisitiza wananchi kulima kilimo ambacho kitaleta manufaa kwao.




Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akikagua shamba la Mihogo 


Mkuu wa wilaya ya Geita akikagua shamba la pamba

Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimpongeza mkulima wa pamba ambaye alipendezwa na maendeleo ya shamba lake.


Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi amewataka maafisa kilimo na umwagiliaji kufanya tathmini halisi ya mazao  yanayoweza kustawi kwenye maeneo tofauti na mazao watakayobaini kuwa yanastawi vizuri wawahimize wananchi kuyalima

Mwl Kapufi amesema hayo wakati akiwa kwenye zoezi la kukagua mashamba ya pamba ,mtama na Mihogo kwenye Kata ya Kaseme na Magenge Wilayani Humo.

Amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya Hali ya Hewa ni vema maafisa kilimo wakatembelea maeneo na kuangalia  aina ya mazao yanayostawi

 “Kwa wilaya yetu ya Geita Halmashauri ya Wilaya na Halmashauri ya Mji natoa wito kwanza kwa maafisa kilimo na umwagiliaji wote waweze kufanya tathmini halisi ya mazao ambayo yanatakiwa kustawi katika eneo husika, hayo mazao ambayo yatastawi kwenye maeneo hayo ndiyo tuwahimize wananchi waweze kulima kwenye maeneo hayo”Alisema Kapufi.


Hata hivyo wakulima  wa zao la pamba katika kijiji cha Katangalo kata ya Kaseme wamemwambia Mkuu wa wilaya kuwa kukosekana kwa pampu za kutosha kwa ajili ya kunyunyuzia dawa kunasababisha uharibifu mkubwa  wa zao hilo la kibishara kwani kwa sasa wakulima takribani 300 wanatumia pampu moja ambayo haitoishi kwa mahitaji yao.


Akijibu kero hizo Mkuu wa Wilaya Mwalimu Herman Kapufi, amewataka watendaji wa serikali za  vitongoji na Vijiji kuwa na mfumo mzuri wa kubainisha changamoto za wakulima ili zipatiwe ufumbuzi.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE 0755550391 GEITA TANZANIA.

Share it:

habari

Post A Comment: