Na
Lulu Mussa
Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, hii leo amekutana na taasisi zizohusika
na uratibu na usimamizi wa kemikali hapa nchini.
Akiongea na Taasisi
hizo, Waziri Mpina amewaagiza watendaji hao kudhibiti na kusimamia kemikali
hatarishi nchini ikiwa ni pamoja na kuratibu usafirishaji, usambazaji na
matumizi ya kemikali hizo hapa nchini kwa namna bora zaidi.
Waziri Mpina
amezitaka taasisi hizo kutoa taarifa za utendaji wa kazi kila robo ya mwaka kwa
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimizi wa Mazingira kwa mujibu wa Sheria ya
Mazingira kifungu namba 170.
“Nawaagiza kuwasilisha takwimu za kemikali
zinazozalishwa nchini, zinazoagizwa au kusafirishwa nje ya nchi, pamoja na kuainisha
viwanda vinavyozalisha kemikali vilivyosajiliwa na maghala yaliyosajiliwa
kuhifadhi kemikali hizo” alisisitiza Mpina.
Katika kikao hicho
Waziri Mpina pia ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
nchini ndani ya miezi miwili kuandaa muongozo na kuupitisha katika hatua zote
wa namna bora ya kuteketeza taka hatarishi bila kuathiri mazingira.
Aidha Waziri Mpina
ameagiza kuandaliwa kwa andiko litakalobainisha umuhimu wa kuteketeza taka
hatarishi. “Kama taifa ni lazima tuwe na “dedicated Incinerator” kubwa kutekeza
taka hizo hatarishi kwa kuzingatia taka zinazozalishwa hapa nchini” Mpina
alisisitiza.
Katika hatua
nyingine, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini, Wakala
wa Maabara ya Veterinari Tanzania, Tume ya Nguvu za Atomiki, Taasisi ya Utafiti
ya Viuatilifu katika Kanda za Kitropiki, Mamlaka ya Chakula na Dawa, OSHA na
Mkemia Mkuu wa Serikali kwa pamoja wametakiwa kuanda Hati ya Makubaliano ya
kuratibu utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuhuisha Sheria zao na
kuleta mapendekezo Serikali ya vifungu vya kufanyiwa marekebisho.
Taasisi alizokutana
nazo ni pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini
(NEMC), Taasisi ya Nguvu za Atomiki, Mamlaka ya Chakula na Dawa na Mkemia Mkuu
wa Serikali.
Post A Comment: