Mwenyekiti wa watunza mazalio na makulio ya samaki Bashiri Manampa kutoka Mwaro wa Nyamilembe wilayani Chato mkoani Geita amewashukuru wenyeviti wenzake wa miaro ya Buhungu na nyakakarango kwa kufungua mipaka ili kukomesha uvuvi haramu ndani ya ziwa victoria.
Akizungumza na Maduka online ofisini kwake Bw. Manampa Alisema kuwa ni muda mrefu amekuwa akiwaomba wenyeviti hao kufungua mipaka waliyokuwa wamejiwekea hali ambayo ilipelekea wavuvi haramu kutumia mipaka hiyo kujificha na kukwepa doria ya majini.
"Kiukweli kufunguliwa kwa mipaka ambayo wavuvi haramu walikuwa wakitumia mwanya huo kujificha imesaidia sana kwani kwasasa tumedhibiti hali hii ya uvuvi haramu kwa asilimia kubwa"Alisema Manampa.
Katika hatua nyingine Bw. Manampa ameongeza kuwa kutokana na ushirikiano huo watapunguza au kuondoa suala la uvuvi haramu ambalo limekuwa na changamoto nyingi wilayani humo.
Aidha hivi karibuni waziri wa kilimo ,uvuvi na mifugo Dkt Charlse Tizeba alifika wilayani humo na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo ambapo alitoa onyo kali kwa watu wanao jihusisha na uvuvi haramu ikiwa ni pamoja na kuongeza adhabu kwa mtu atakae bainika anajihusisha na vitendo hivyo
Baadhi ya wananchi wa nyamirembe na nyakakarango Bw: Ganyanka Matele na Edward Magafu wameipongeza serikali kwa jitihada za kupambana na matumizi ya zana haramu za uvuvi ikiwa ni njia ya kutokomeza uvuvi haramu hapa nchini.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: