Wakati ligi kuu Tanzania bara ikielekea ukingoni, Yanga ndio timu ambayo ipo kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu ukilinganisha na wapinzani wao Simba. Yanga inaongoza ligi kwa wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa lakini wakiwa sawa kwa pointi na Simba wote wakiwa na pointi 62.
Yanga imebakiza mechi tatu kabla ya ligi kumalizika, mechi hizo ndio zitawapa ubingwa au kuwanyima ubingwa. Ikiwa watashinda mechi zote watafikisha pointi 71 pointi ambazo hazitafikiwa na Simba hata kama watashinda mechi zao mbili zilizobaki ambazo zitawafanya wafikishe pointi 68.
Kwa hiyo mechi tatu za Yanga zilizosalia ndio zimeshikilia ubingwa wa 2016-17, ambao kama watautwaa itakuwa ni mara yao ya tatu mfululizo tangu walipochukua msimu wa 2014/2015, 2015/2016 na msimu huu 2016/2017 kama watafanikiwa kuuchukua.
Mechi za Yanga zilizosalia ni:
Yanga vs Mbeya City
Yanga vs Toto Africans
Mbao vs Yanga
Yanga imepoteza mechi tatu tu tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi, sare tano huku ikiwa imeshinda mara 19 kati ya mechi 27 walicheza hadi sasa. Timu sita zimeichangia Yanga pointi sita kila moja kwa maana ya kufungwa mechi mechi zao mbili za nyumbani na ugenini,timu nne zikaichangia pointi nne baada ya kukubali kufungwa mechi moja na mechi nyingine kutoka sare, zipo pia ambazo zimeshachangia pointi tatu kwa maana kwamba zilishinda mechi mechi moja na kufungwa nyingine huku nyingine zikisubiri mechi zao za marudiano.
Lakini zipo zilizochangia pointi moja tu, hii ni baada ya kutoka sare mechi mmoja halafu wakashinda mechi nyingine.
Mbio za ubingwa wa Yanga zimechagizwa na Tanzania Prisons, Majimaji FC , Mwadui FC, Ruvu Shooting, Kagera Sugar na JKT Ruvu ambazo zote zimeipa pointi sita , timu ambazo zimeipa Yanga pointi nne ni pamoja na Ndanda FC, African Lyon, Mtibwa Sugar, Azam FC. Yanga imepata pointi tatu kutoka kwa Toto Africans, Mbao FC, Stand United huku ikiambulia pointi moja kwa Simba SC.
|
Navigation
Post A Comment: