WANAFUNZI WATATU WAFA MAJI GEITA

Share it:
Baadhi ya viongozi wa kiserikali na wakidini pamoja na wananchi wakiwa kwenye ibada ya mazishi ya  watoto watatu ambao wamekufa maji .

Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita waki shuhudia miili ya marehemu .

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akitoa pole kwa wafiwa wa tukio la watoto watatu ambao wamekufa kwenye maji ziwa Viktoria.

Mkuu wa Mkoa wa  Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga  akitoa pole kwa wafiwa wa tukio la watoto watatu ambao wamekufa kwenye maji ziwa Viktoria.

Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye eneo la tukio.

Usafiri wa Boti ambao wamekuwa wakitunmia wanakijiji wa Kisiwa cha Lulegea ambacho ndio kiliwaacha wanafunzi kabla ya tukio kutokea.

 Baadhi ya abilia wakishuka kwenye kivuko hicho.

Mkuu wa Mkoa wa  Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga  akizungumza na wananchi wa Kisiwa cha Lulegea.

Baadhi ya watoto ambao wamenusurika wakati wa dhoruba ambalo lilitokea



MATUKIO YOTE YA PICHA NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLINE

Kufuatia tukio la wanafunzi 24 kuzama maji  ziwa viktoria na wengine watatu kupoteza maisha wakati wakitokea masomoni  Kijiji cha Butwa na wakielekea    Kitongoji cha Lulegea  Kata ya Izumacheli Wilaya na Mkoa wa Geita,Mkuu wa Mkoa huo Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ameagiza halmashauri ya Wilaya pamoja na wananchi wa kijiji hicho kuwa na  ushirikiano ili kujenga shule kwenye kisiwa hicho.

Hayo ameyasema wakati alipokuwa akitoa pole kwa wafiwa na jamii ambayo ipo kwenye kisiwa hicho kutokana na tukio la kufariki kwa wanafunzi watatu wa shule ya msingi Butwa wakati wakitokea shule kurudi Nyumbani.

Mh,Kyunga amesema kuwa ili kuwasaidia wananchi wa Kitongoji cha Lulegea hawana budi kujenga shule na kwamba wakati utakapokuwa umetulia wa mvua ni vyema kwa wananchi kujumuika kwa pamoja na kushirikiana ili waweze kujenga shule ambayo itawasaidia wananfunzi.

“Mimi  pia nimesikitishwa sana na msiba huu wa wanafunzi hawa lakini ni muhimu kutafuta suluhisho la matatizo haya kwa  wanafunzi  na suluhisho ni serikali na nyie wananchi kujitokeza kuchangia nguvu ili tuweze kujenga shule kwenye eneo hili ili matatizo ya namna hii yasiweze kujirudia tena siku nyingine”Alisema Kyunga.

Tululaza Kurulahenda ambaye alikuwa amewabeba wanafunzi hao kwenye Mtumbwi ambao ulizama ameelezea kuwa chanzo ambacho kilisababisha ajali hiyo ni kutokana na  watoto kutokutulia wakati akiendesha mtumbwi  pamoja na hali kutokuwa shwari ya ziwani.

“Muda ulikwenda sana na boti ambayo huwa inawabeba wanafunzi ilikuwa imekwisharudi  moja kati ya mama ambaye mtoto wake amefariki akaniomba niwafuate na mtumbwi namimi sikubisha kwakuwa walikuwa ni watoto ikabidi niwafuate kwa bahati mbaya wakati ninarudi nikiwa nimekaribia kufika upande wa pili hali iliharibika na kukawepo na upepo hali ambayo ilipelekea wanafunzi kuanza kupiga kelele na kuruka lakini hata hivyo mimi pamoja na mwanafunzi ambaye anaitwa Tisekwa tulianza juhudi za kuwaokoa wengine ndipo  na tukawa tumefanikisha baada ya baadhi ya wavuvi wenzangu kuja kutusaidia na tulipowaokoa tukagundua kuwa watatu hawaonekani ndipo tukaanza mchakato wa kuwatafuta baada ya juhudi majira ya saa moja tukaupata mwili wa mwanafunzi mmoja akiwa amefariki wengine tumewapata asubuhi”Alisema huku akiwa na masikitiko Tululaza.

Aidha Tisekwa Gamungu ambaye ni mtoto aliyewaokoa wenzake amesema kuwa walikuwa wakitoka shuleni  wakati wakiwa njiani  wakirudi waliona kama kimbunga kimetokea hali ambayo ilipelekea wengi wao kulia huku wakiombwa kurudishwa kule ambako wametokea.

Wanafunzi ambao wamepoteza maisha kwenye tukio hilo ni Kumbuka Bruno Thomas (13) ni mwanafunzi wa darasa la tano  ,Anastazia Christopha (12)darasa la tatu na Sophia Muungano (11)darasa la pili .

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE .

Share it:

matukio

Post A Comment: