MAHAKAMA INAYOTEMBEA YAANZA KUWASAKA WACHAFUZI WA PAMBA.

Share it:

Mkaguzi wa bodi ya pamba wilayani maswa mkoani simiyu Ally Maborouk akiongoza operesheni ya kukagua pamba kwa kutumia mahakama inayotembea katika vituo mbalimbali vya kununulia pamba wilayani humo.


Na COSTANTINE MATHIAS, Maswa.


Bodi ya Pamba Tanzania wilayani Maswa mkoani Simiyu imefanya operesheni maalumu ya kuwagakua wanunuzi na wauzaji wa Pamba ambao wamekuwa wakichafua  zao hilo kwa  kuichanganya mchanga, maji na udongo ili kuongeza uzito na kupata faida mara mbili ambapo katika huku oporesheni wakulima na wanunuzi wamepongeza zoezi hilo linaloondoa udanganyifu katika zao hilo.


Wakiongea katika ukaguzi huo baadhi ya wanunuzi na wakulima katika vijiji vya Mwabayanda na Nguliguli walisema kuwa zoezi hilo ni zuri kwa sababu linawafanya wajitathini na kufahamu ubora wa pamba wanayoinunua pia kuwakumbusha wakulima kutoharibu pamba yao.


‘’zoezi hili tunaomba liwe endelevu kwa sababu linagusa wakulima na wanunuzi kuwa yoyote atakayekutwa na kosa anahukumiwa hapohapo, litaondoa uchafuzi wa pamba na kuongeza ubora wake hivyo litakuza soko la pamba kimataifa ambayo awali ilikuwa imeshuka kutokana na pamba yetu kuwa chafu’’ alisema Nkuba Minoja.


John Ng’hona alisema kuwa pamoja na ukaguzi huo, katika msimu ujao watuletee  mbegu ya pamba na pembejeo kwa wakati ili tuweze kulima kwa uhakika na kuongeza uzalishaji.



Naye Mkaguzi wa Bodi ya Pamba wilayani humo Ally Maborouk alisema kuwa zoezi hilo ni endelevu na wanunuzi wanaoharibu pamba ni bora watafute biashara nyingine kwa kuwa bodi hiyo inasimamia wauazaji na wanunuzi na kuhakikisha pamba inayozalishwa na kuuzwa ni safi.


‘’wanunuzi wanaoharibu pamba ni bora watafute biashara nyingine, tutahakikisha pamba yote inayozalishwa na kuuzwa ni safi ili isiharibu soko la zao hilo kimataifa, tuko imara tutahakikisha tunawashughilikia ipasavyo’’ alisema Maborouk.


Aidha katika zoezi hilo lilioambata na mahakama  inayotembea (mobile court) imekagua vituo vya pamba katika vijiji vya Nguliguli, Mwabayanda, Ilimbambasa, Senani, Zebeya na Mwabadimi na kuibua hoja baada ya mnunuzi mmoja wa pamba kampuni ya Gaki kijiji cha Igumangobo kufunga kituo na kuwakimbia wakaguzi hao.


Baada ya kuona hali hiyo Mkaguzi wa Pamba aikifunga kituo hicho na kumwagiza mtendaji wa kijiji kumkamata mnunuzi huyo ili aweze kueleza sababa zilizomfanya akikimbie kituo chake.


Katika kijiji hichohicho cha Igumangobo wanunuzi wawili Malugu Sungwandeba na George Salum wanunuizi wa pamba Kampuni ya Kahama Cotton Co Ltd ya mjini Kahama mkoani Shinyanga walipatikana  na hatia baada ya kukiri kukutwa wamenunua pamba chafu katika ghala lao


Katika mahakama hiyo inayotembea Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Nyalikungu,Lilian Kinyemi aliwahukumu washitakiwa hao adhabu ya kifungo cha miezi mitatu jela kila mmoja au kulipa faini ya Sh 50,000 na Kampuni hiyo kuilipa bodi ya Pamba Sh 500,000 na washitakiwa walilipa faini zote na kuachiwa huru.

Share it:

habari

Post A Comment: