MSUKUMA NA MADIWANI SABA WAPANDISHWA KIZIMBANI NA KUSOMEWA MASHITAKA MANNE.

Share it:
Mbunge wa Jimbo la Geita ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Geita Joseph Kasheku Msukuma akiwapungua Mkono wananchi ambao walikuwepo nje ya mahakama baada ya  kutoka  ndani ya mahakama ya hakimu Mkazi Mkoani Geita kwa dhamana ya Sh,Milioni Tano pamoja na viongozi wengine.

Mbunge wa Jimbo la Geita Joseph Kasheku Msukuma ambaye yupo katika kati na kulia kwake ni Diwani wa Mtakuja Constatine Morandi wakiwasili Kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi.

Mbunge Msukuma akisalimiana na wananchi wakati akilipokuwa akiingia ndani ya mahakama.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita,Bi Khadja Said na Diwani wa viti maalum kwenye Halmashauri Hiyo Bi,Mahimuna Mingisi wakiingia ndani ya mahakama.

Mbunge Msukuma akitoka Nje ya mahakama baada ya kupatiwa dhamana.




PICHA NA JOEL MADUKA.




Mbunge wa Jimbo la Geita Joseph Msukuma na madiwani 7 wa halmashauri ya Mji wa Geita na ile ya Wilaya ya Geita pamoja na mwananchi mmoja wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita na kusomewa mashitaka manne yanayowakabili.

Washitakiwa wengine waliofikishwa mahakamni hapo ni Madiwani Costantine Morandi, Winifrida Malunde, Ngudungu Joseph, Martin Kwilasa, Hadija Said, Michael Kapaya, Maimuna Mengisi na Steven Werema ambaye ni mwananchi.

 Mbele ya hakimu Mkazi mfawidhi Ushindi Swalo, upande wa mashitaka ukiongozwa na mawakili wa Serikali, Emily Kiria na Hezron Mwasimba, Wakili Hezron amesema Septemba 14 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi washitakiwa hao wanadaiwa kufanya mkutano usio halali, kula njama, kuziba barabara na kuharibu Bomba la maji kutoka Ziwa Viktoria kwenda kwenye mgodi wa GGM.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, washitakiwa wote wamekanusha kuhusika na vitendo hivyo na wameachiwa kwa dhamana ya Sh Milioni 5 huku kila mshitakiwa akitimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja
Aidha kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 10 mwaka huu.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.


 
Share it:

matukio

Post A Comment: