WAFANYABIASHARA WAASWA KUTOPANDISHA BEI WAKATI WA MWEZI WA RAMADHAN

Share it:
Wafanyabiashara wakiendelea na shughuli ya kuzaa bidhaa ambazo zimekuwa zikitumika zaidi karika Mfungo wa mwezi wa Ramadhani kwenye soko la Nyankumbu Mjini Geita.


Sheikh Mkuu wa wilaya ya Geita, Sheikh Adam Santuri  Akizungumza juu ya wafanyabiashara kutokupandisha Bei ya vyakula katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi mtukufu wa ramadhani.

Waislam Duniani kote leo wameanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na kumekuwa na kawaida ya kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali zinazotumiwa wakati wa mfungo huo.

Kutokana na hilo, Wafanyabiashara Wilayani Geita wametakiwa kutopandisha bei ya bidhaa hizo kwa kuwa wanaweza kuathiri funga kwa baadhi ya Waislam wasio na uwezo.

Sheikh Mkuu wa wilaya ya Geita, Sheikh Adam Santuri amesema ni vyema wafanyabiashara wakaendelea na bei ya kawaida kwa vyakula hivyo na kwa kuzingatia bei elekezi iliyopangwa na serikali.

Baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Nyankumbu Mjini Geita wamesema wanalazimika kupandisha bei kwa kuwa nao wananunua bidhaa kwa bei ya juu kutoka kwa wakulima  ambao wamekuwa wakitoa mashambani.

Baadhi ya Waislam wamesisitiza waislam wenzao kutokatishwa tamaa na kupanda kwa bei za bidhaa bali waendelee kutekeleza nguzo ya nne kati ya 5 za uislam kwa kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Share it:

BIASHARA

Post A Comment: