Mwanasheria wa Shirika la The Golden line Bi, Walta Carlos akizungumza kwenye mdahalo huo. |
Baadhi ya madiwani wakimsikiliza Muongozaji wa mdahalo huo.
Utafiti uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali la The
Golden line umebaini kuwa wanawake wengi Mkoani Geita wanaogopa kuwania nafasi
mbalimbali za Kisiasa na kijamii wakihofia kushindwa pamoja na mila potofu.
Shirika hilo limeeleza kuwa wanawake wengi wanaogopa kuwania
uongozi kwenye Nyanja hizo wakidai kutoaminiwa na jamii pamoja na dhana potofu
kuwa kazi ya Mwanamke ni kulea familia.
Akizungumza kwenye mdahalo uliwashirikisha Madiwani wa Halmashauri tano( 5 )za mkoa wa
Geita kwenye ukumbi wa Kanisa Anglikana mjini Geita, Mwanasheria wa Shirika
hilo Bi Walta Carlos amesema mila potofu ni kikwazo kwa wanawake kuwania nafasi
za uongozi kwenye siasa.
“Wakati tukiendelea na tafiti zetu licha ya kwamba wanawake
wengi wanauogo lakini pia tumebaini kuwepo kwa mila potofu kwa maana kwamba
mama akiwa kiongozi aweze kusimamia vyema familia yake na kufanya majukumu ya
msingi kama mwanamke hivyo kwa upande wa baadhi ya wanaume wameendelea
kuwakataza wake zao kuwania nyadhifa mbali mbali kutokana na kuwepo kwa dhana
hiyo”Alisema Bi,Walta.
Aidha Diwani wa Kata ya Lwamgasa Bw Josepha Kaparatusi
amesema wanawake wanayo nafasi sawa na wanaume kuwania uongozi hivyo hawapaswi
kuogopa na kwamba ni vyema wakajitambua na kujitokeza na kuachana na tabia ya
kuendelea kujificha.
Baadhi ya viongozi wanawake waliozungumza na mtandao huu,wamesema wanapowania nafasi hizo
wamekuwa wakikumbana na vikwazo mbalimbali ikiwa ni pamoja na baadhi ya jamii
kuwaona kuwa awanauwezo wa kuongoza.
|
Post A Comment: