Sehemu ya mfuniko wa choo ikiwa imejaa na kusababisha maji machafu kutoka nje kwenye Soko la Nyankumbu Mjini Geita. |
Maji machafu yakitililika kutoka kwenye chemba ya choo hicho. |
Diwani wa Kata ya Nyankumbu Michael Kapaya akielezea juu ya jitihada za kukitapisha choo hicho kutokana na kujaa. |
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Bw Majagi Maige akizungumzia juu ya hatua ambazo wamekwisha kuzichukua za kukitapisha choo cha Soko la Nyankumbu. |
Wafanyabiashara kwenye soko la Nyankumbu mjini Geita
wamelalamikia kero ya kujaa kwa choo kwenye soko hilo.
Wakizungumza na mtandao huu wafanyabiashara hao wamesema
hali hiyo inasababisha maji taka kuchuruzikia kwenye maeneo wanayofanyia
shughuli zao.
Baadhi ya wafanyabiashara wamesema licha ya kuwa wanalipa
Shilingi mia mbili ( 200 )kwa ajili ya kupata huduma hiyo lakini bado mamlaka
husika imekitelekeza choo hicho kutokana na kujaa kwa muda mrefu hali inayoweza
kusababisha magonjwa ya mlipuko.
“Tupo hatarini kufa kutokana na magonjwa ya mlipuko kutokana
na hali hii ya choo kwani maji haya yamekuwa yakitawanyika na kuja kwenye
maeneo yetu ya biashara husuani kwenye kipindi cha mvua ambazo zinaendelea
kunyesha hali ni mbaya sana tunaomba mamlaka itusaidie jamani maana tunaangamia
na hali hii yani tunakuwa kama sio wafanyabiashara wa soko la mjini halmashauri
kuna gari ni kitendo cha kusema tu mkurgenzi gari lije linyonye hiki kinyesi
tunaomba waandishi mtusaidie”Alisema Bw,Kasiusi Michael.
Baadhi ya wananchi wamesema wanakerwa kwa kujaa kwa choo
hicho na kuitaka Halmashauri ya Mji wa Geita kulishughulikia tatizo hilo.
“Hali hii ni mbovu tunapopita hapa pananuka na maji haya
yanaelekea sehemu ambapo wafanyabiashara wa mboga mboga wanapooshea lakini
jambo la kushangaza ingekuwa ni sisi wananchi tunachoo cha namna hiyo
tungekamatwa badala ya halmashauri kuonesha mfano yenyewe ndio imekuwa chanzo
cha kuachaniza mazingira kama haya ya choo kuwa machafu”Alisema Bi Sophia
Madinda.
Diwani wa Kata ya Nyankumbu Bw Michael Kapaya amesema
watachimba shimo jingine la choo pembeni lakini kutokana na mvua zinazoendelea
kunyesha imeshindikana hadi zitakapopungua.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Bw Majagi Maiga
amesema wamechelewa kupata taarifa lakini tayari wamepeleka gari kwa ajili ya
kunyonya maji taka.
Post A Comment: