Naibu Waziri wa Elimu William Ole Nasha kizungumza kwenye mahafari ya Tatu ya shule za wavulana na wasichana za Sekondari ya WAJA Mjini Geita. |
Mkurungenzi wa WAJA ,Chacha Wambura akiserebuka Nyimbo ya kikabila kutoka Mkoa wa Mara na Meneja wa WAJA Bi,Jacqueline Tesha wakati wa sherehe za mahafari ya Tatu ya kidato cha Sita. |
Wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule ya wasichana ya Waja Sekondari wakifuatilia matukio mbali mbali yaliyokuwa yakiendelea. |
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na wazazi wakifuatilia Burudani mbali mbali zilizokuwa zikiendelea. |
Wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule ya wavulana ya Waja Sekondari wakifuatilia matukio mbali mbali yaliyokuwa yakiendelea. |
Meneja wa WAJA Bi,Jacqueline Tesha akizungumza na wanafunzi juu ya kuwa na nidhamu kipindi chote ambacho watakuwa mitaani. |
Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale Hamim Gwiyama akuzungumza na wanafunzi juu ya umuhimu wa kukabiliana na maadui watatu. |
Mkurugenzi wa Waja Bw ,Chacha Wambura akielezea changamoto ambayo imekuwa ikisababisha kupandisha hada shuleni hapo. |
Naibu Waziri wa Elimu William Ole Nasha amesema kuwa
serikali inatambua mchango wa sekta
binafisi na kwamba itaendelea kuziunga mkono hili ziweze kufanya shughuli zao
kwa wapesi zaidi.
Hayo ameyabainisha katika mahafari ya tatu ya shule ya
sekondari ya wasichana na wavulana ya Waja iliyopo Mkoani Geita.
Ole Nasha amewaonyo
watu ambao wamekuwa wakisema kuwa serikali ya awamu ya tano haitambui mchango
wa sekta binafisi na kwamba suala hilo sio la kweli kwani sekta hiyo ni ya
muhimu kwa kuendelea kuinua kipato cha Taifa.
“Idadi ya shule za binafsi na vyuo zimekuwa
zikiongezeka siku hadi siku hivyo napenda kuwahakikishia kuwa serikali
itaendelea kushirikiana na sekta binafisi kuboresha mazingira ya elimu nchini”Alisema
Ole Nasha.
Nae Kaimu Mkuu wa
wilaya ya Geita ambaye ni Mkuu wa Wilaya
ya Nyang’hwale Hamim Gwiyama ametaja maadui ambao wameendelea kulitafuna Taifa
na mbinu ambazo zinatakiwa kufanyika ili kuwashinda maadui hao.
“Baba wa Taifa hayati Mwl Julius Nyerere aliwai kusema
maadui ya Taifa ni Ujinga maradhi na umasikini kwa hiyo ukiwa na maadui unaenda
vitani na ukiwa vitani uchagui silaha hivyo serikali yetu aichagui silaha kwani
maamuzi ambayo yanafanywa na serikali yanalengo la kusaidia kumshinda adui
ujinga na wazazi ambao mnakubali watoto wenu kuingia kwenye shule hizi mnafanya
jambo la maana sana”Alisema Hamim Gwiyama.
Sanjali na hayo Meneja wa WAJA Bi,Jacqueline Tesha amewataka wahitimu hao kuwa na sifa njema
pindi watakapokuwa mitaani ikiwa ni pamoja na kuwa na maadili mema ambayo
wamefundishwa shuleni hapo.
Aidha Mkurugenzi wa Waja Bw ,Chacha Wambura amemuomba Naibu
waziri wa Elimu kuwasaidia suala la kodi kutokana na kulipa sawa na watu ambao
wanafanyabiashara za mahoteli jambo ambalo sio sawa kutokana na kwamba taasisi
hiyo inajishughulisha na utoaji wa elimu.
Kufuatia maombi hayo Mgeni rasimi Naibu waziri wa elimu
amehaidi kushughulikia tatizo hilo kwenye ngazi husika.
Post A Comment: