Rais
John Magufuli ameagiza kusitishwa kwa ubomoaji wa nyumba za wananchi
zaidi ya 2,000 wanaodaiwa kuvamia eneo la Uwanja wa Ndege Mwanza, kituo
cha polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ).
Akizungumza
na wananchi wakati uzinduzi wa daraja la juu la waenda kwa miguu eneo
la Furahisha jijini Mwanza leo Jumatatu, Rais Magufuli ameagiza ubomoaji
huo usitishwe hadi atakapotolea uamuzi suala hilo.
“Rais
ndiye msimamizi mkuu na mwenye mamlaka juu ya ardhi yote nchini; hawa
(wananchi) ndio walionipa urais," amesema Rais Magufuli.
Agizo
la Rais Magufuli anayefanya ziara ya siku mbili mkoani Mwanza
limetokana na mabango ya wananchi kutoka maeneo ya Kayenze, Muhoze na
Kigoto wakielezea kero zinazowakabili ikiwemo tishio la nyumba zao
kubomolewa kwa madai ya kuvamia maeneo ya ndege, jeshi la polisi na JWTZ
Rais
amewaagiza mawaziri wanne kutoka Wizara za Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi, Mambo ya Ndani, Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ulinzi
na Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
kukutana kujadili na kutoa mapendekezo ya namna ya kutatua mgogoro huo
ndani ya siku 21 kunazia leo Jumatatu.
Amesema
baada ya mapendekezo ya vikao vya mawaziri hao, ataangalia namna ya
kushughulikia suala hilo, hata kama itabidi kubadilisha sheria kulinda
maslahi ya wananchi ambao baadhi wameishi maeneo hayo kwa zaidi ya miaka
30.
Katika
hotuba yake, Rais pia ameahidi kukamilisha malipo ya Sh9 bilioni
yanayodaiwa na mkandarasi anayetekeleza mradi wa upanuzi wa Uwanja wa
Ndege wa Mwanza kwa kiwango cha kimataifa ili ukamilike kabla ya mwaka
2020.
Post A Comment: