|
Mtoto ambaye anatatizo la mdomo sungura akisubilia kwenda kufanyiwa matibabu Jijini Mwanza wakati wa hafla ya kuwaaga. |
|
Mratibu
wa kitengo cha afya Mgodini GGM Dkt.Kiva Mvungi akisisitiza jamii kutokuwa na dhana ya kuwatenga na kuwanyanyapaa watoto ambao wanakuwa na matatizo ya midomo sungura. |
|
Meneja
mahusiano kwa jamii wa Mgodi wa GGM
Bw.Manase Ndoroma akielezea namna ambavyo wameendelea kuendesha zoezi la kutoa msaada wa matibabu kwa watoto wenye tatizo la mdomo sungura tangu mwaka 2004. |
|
Mkurugenzi mkuu wa Mgodi wa GGM Richard Jordinson,akielezea juu ya gharama ambazo wametumia hadi sasa tangu walipoanza mpango wa matibabu kwa watoto ambao wanamidomo sungura. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwapa maneno ya faraja wakati alipokuwa akiwaaga watoto pamoja na wazazi ambao wanatarajia kwenda mwanza kwaajili ya matibabu. |
|
Mkurugenzi mkuu wa Mgodi wa GGM Richard Jordinson na Mratibu
wa kitengo cha afya Mgodini GGM Dkt.Kiva Mvungi wakimsikiliza mkuu wa Wilaya. |
|
Watoto wenye tatizo la midomo sungura wakiwa na mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mkuu wa mgodi wa GGM kwenye picha ya pamoja. |
|
(PICHA NA JOEL MADUKA)
Mkuu wa wilaya ya Geita
,Mwl Herman Kapufi amewataka wazazi na walezi wenye watoto ambao wanamatatizo ya midomo
Sungura,Mtindio wa ubongo na ulemavu mwingine kutowanyanyapaa watoto wao badala
yake kuwatolea taarifa kwa wataalamu wa afya ili serikali iwatambue nakuwatafutia
matibabu.
Hayo
aliyasema wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watu
wenye matatizo ya midomo Sungura wanaosafiri kwenda jijini Mwanza kupatiwa
Matibabu ambayo yanadhaminiwa na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM).
Mkuu wa wilaya alisema matibabu ya watu hao
yanafadhiliwa na mgodi wa dhahabu wa Geita GGM kwakushirikiana na Shirika moja
la Australia liitwalo Rafiki Mission hivyo ni vyema kwa jamii pindi wanaposikia
matangazo kujitokeza kwa kuwapeleka watoto wao au ndugu zao kujiandikisha
kwaajili ya kupatiwa matibabu.
Akitoa taarifa ya
Mkurugenzi wa Mgodi wa GGM Richard Jordinson kuhusu matibabu ya watu hao,
Meneja mahusiano kwa jamii wa Mgodi wa
GGM Bw.Manase Ndoroma alisema tangu kuanzishwa kwa Mpango huo wa matibabu
kwa watu wenye midomo ya sungura mwaka 2004, Mgodi wa GGM umetumia kiasi cha
shilingi Bilioni 1 hadi sasa.
Bi.Mwajuma Morris, ni mmoja
wa wazazi wenye watoto waliozaliwa na tatizo la mdomo Sungura ambao ni miongozi
mwa watoto wanaosafirishwa kwenda Hospitali ya Seketule Jijini Mwanza kwaajili
ya matibabu ameelezea kuwa mtoto wake amekuwa akitengwa na jamii na muda
mwingine watoto wenzake wamekuwa wakimcheka anapokuwa shuleni hali ambayo
inamfanya kujiona ananyanyapaliwa na jamii ambayo inamzunguka.
Kwa upande wake mratibu wa
kitengo cha afya Mgodini GGM Dkt.Kiva Mvungi aliwataka wananchi kujiepusha na
vitendo vya unyanyapaa kwakuwa tatizo hilo sio laana.
Post A Comment: