Chama cha
Waandishi wa Habari wa
Kupiga Vita Matumizi
ya Dawa za Kulevya na Uhalifu
Tanzania(OJADACT), kimeungana na Waandishi
wa Habari, wadau na wanafamilia
wa Mwandishi wa Habari Bwana Azory Gwanda , anayefanya kazi na
Mwananchi Communications Ltd
Mkoa wa Pwani, kulaani tukio la
kushikiliwa kwake na watu wasiojulikana, kuanzia Alhamis Novemba 30, 2017 hadi
sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari
kwenye ofisi za chama hicho Mwenyekiti wa OJADACT Bw,Edwin
Soko amemwomba Mkuu wa
Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro,
kufuatilia kwa ukaribu
tukio la kupotea kwa Mwandishi huyo na
kuhakikisha anapatikana akiwa salama, pia tunawaomba watanzania kuwa watulivu wakati Jeshi la
polisi lkitekeleza wajibu wake.
Soko ameongeza kuwa OJADACT inaamini kwenye kuheshimu
haki za binadamu kupitia katiba
ya Nchi, Ibara ya
14 inaanisha kuwa, “kila mtu ana
haki ya kuishi na kupata toka kwa
jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria” Hivyo kila mtu anastahili kuishi na kuwa salama.
Pia ametoa rai kwa wamiliki wa
Vyombo vya Habari Nchini, kuwa na
mifumo ya kisasa ya ulinzi kwa
Waandishi wao, pamoja na Mwandishi
mmoja mmoja kujifunza
mbinu za viashiria hatari,
(Security alert detection), ili kujilinda.
Na kwamba chama hicho, kinafuatilia
kwa ukaribu suala hilo kwa kushirikiana na Vyombo vya ulinzi na usalama, Kampuni ya
Mwananchi Communications LTD, Wanahabari,
na wadau wote wa
Habari Nchini kujua kujua mustabali wa Mwandishi Azory Gwanda.
|
Navigation
Post A Comment: