![]() |
Moja kati ya madarasa ya shule ambayo mkuu wake analalamikiwa na wananchi kuwatoza michango mbali mbali.
Na,Joel Maduka,Geita
|
Wazazi na
walezi wa mtaa wa Moringe Kata ya Buhalahala Wilayani Geita wamemtuhumu mwalimu
mkuu wa shule ya msingi ya 14 kambarage kwa kuwarudisha wanafunzi nyumbani
kutokana na kutotoa fedha za mchango shuleni hapo.
Tangu
Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani chini ya Rais Dr John Pombe
Magufuli kupitia wizara ya elimu, sayansi na ufundi ilitoa waraka wa elimu bure
kuanzia elimu ya msingi mpaka kidato nne.
Akizungumza
na mtandao huu,Bi Odest Timoth alisema kuwa wamekuwa wakitozwa fedha pindi wanapopeleka
watoto wao kuwaandikisha na wanapogoma kutoa wamekuwa wakirudishwa na Mkuu wa
shule na huku wanatambua kuwa serikali
imetoa kibali cha wanafunzi kusoma bure bila ya kutoa pesa hivyo hali hiyo
imeendelea kuwachanganya.
“Hali
hii sio nzuri kabisa serikali imesema
watoto wasome bure leo hii wazazi tunalazimishwa kutoa michango tena pindi tu
unapopeleka mtoto mimi naomba mkuu wa wilaya hatusaidie juu ya huyu mwalimu
maana imeshakuwa ni kero”alisema Bw Peter John .
Diwani wa
Kata ya Buhalahala Bw Mussa Kabese alisema
amekuwa akipokea simu za wazazi wakimlalamikia Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi
14 Kambarage kuwaomba wazazi kiasi cha shilingi elfu kumi na pindi
wanaposhindwa kutoa amekuwa akiwafukuza watoto shuleni hapo jambo ambalo sio
sahihi.
Kufuatia
tuhuma hizo mtandao huu umemtafutta Mwalimu Mkuu Jacob Bossco ambaye ni mwalimu
mteule wa kusimamia shule hiyo akitokea shule ya msingi Mbugani ambapo ,
amekanusha kuhusika na tuhuma hizo na
kuelekeza tuhuma hizo kwa kamati ya ujenzi pamoja na ofisi ya Serkali Mtaa wa
14 Kambarage.
Kutokana na
madai hayo Mkuu wa Wilaya Mwl. herman
kapufi . amepiga marufu kwa Walimu Wakuu wa shule za Sekondari na Msingi
wilayani humo ambao wanajihusisha na
upokeaji wafedha kutoka kwa wanafunzi kama michango na kwamba watakao bainika
watachukuliwa hatua.
Shule hiyo mpya ambayo imejengwa kwa nguvu za
wananchi pamoja na fedha kutoka serikalini bado haijafunguliwa kutokana na baadhi ya miundombinu vikiwemo vyoo
kutokamlika licha ya kuandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza.
Post A Comment: