UKWELI WA MADAI YA SUMU KWA WANAFUNZI GEITA YAJULIKANA.

Share it:
Shule ya EMACO VISION iliyopo Mjini Geita ambayo ndiyo inasadikika mwanafunzi kuwawekea sumu wanafunzi wenzake.


Mzazi wa mtoto anayedaiwa kuwaweka sumu kwenye chakula Bi ,Lidia Charles akizungumza na waandishi wa habari juu ya sakata hilo.

Mwalimu mkuu wa shule , Octavian Laurian akizungumza juu ya namna ambavyo aliweza kuona tukio hilo kama Mwalimu.






Kufuatia taarifa ambazo zilikuwa zimesambaa kwenye mitandaoni ya Kijamii zikimwonesha mwanafunzi wa shule ya msingi ya EMACO VISION ya mjini Geita,  kwa madai alikusudia kuwawekea wenzake sumu kwenye chakula hali hii imezuha hofu na taaruki kwa baadhi ya Wazazi na jamii Mkoani Humo.

Imeelezwa kuwa mwanafunzi wa darasa la nne(Jina linahifadhiwa)alikuwa akicheza na mwezake akiwa na kichupa na alikuwa akichanganya maji na majivu hali ambayo ilipelekea kuruka kwa maji hayo na kwenda kwenye chakula cha mwanafunzi mwenzake ambaye alidai kuwa amewekewa sumu.

Mtandao huu umefanikiwa kufika shuleni hapo na kukutana na Mwalimu mkuu wa shule , Octavian Laurian amesema Julai 20, mwaka huu  wakati wa chakula cha mchana kuna mwanafunzi wa darasa la nne alidai mwenzake ana sumu,na  kwamba walipochunguza walibaini ni maji machafu yaliyokuwa kwenye chupa.

Amesema walimu walipochunguza walibaini ni maji machafu yaliyokuwa kwenye kichupa hicho.

“Watoto walikwenda kuchukua chakula wakiwa kwenye usimamizi wa walimu ,walipokuwa wanakula mmoja alikuwa na kichupa kidogo chenye maji na baadaye walimzunguka wanafunzi wenzake wakidai ni simu lakini tulipochunguza tulibaini kilikuwa na majivu”Alisema Laurian.

Meneja wa shule hiyo ,Edward Bathoromeo amekanusha taarifa ambazo zimezagaa mtandaoni na kwamba suala hilo sio la kweli kwani mtu ambaye amesambaza ujumbe huo alisambaza kwenye group la whatsap la kazini kwake kimakosa kwani baada ya uchunguzi alikili kufanya jambo hilo kimekosa.

Mwanafunzi huyu ambaye anadaiwa kuweka sumu kwenye chakula cha mwanafunzi mwenzake  amesema alichanganya maji na majivu kwa ajili ya kucheza na mdogo wake wanayesoma darasa moja huku mzazi wa mtoto huyo ,Lidia Charles akionesha kusikitishwa na taarifa hizo pamoja na picha ya mwanaye kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Mzazi mwingine , James Leonard amekiri kutuma picha kwenye kundi la WhatsApp la wafanyakazi wenzake huku akikanusha maneno yaliyoko kwenye picha hiyo si ya kwake.
Kamanda wa Polisi Mkoani Humo,Mponjoli Mwabulambo amesema wameunda tume ya uchunguzi ya kufuatilia tukio hilo hili kujua kama kweli chupa hiyo ilikuwa na sumu.

Share it:

habari

Post A Comment: