PICHA MBALI MBALI ZA MAADHIMISHO YA MTOTO WA KIKE MKOANI GEITA

Share it:
Bango likiwa linasomeka uzinduzi wa mradi wa kuzuia ndoa za utotoni wilayani Geita,huku likiwa na kauli mbiu isemayo wezesha mtoto wa kike zuia ndoa za utotoni.

Maandamano ya siku ya mtoto wa kike wakiwa barabarani kuelekea ukumbi wa halmashauri ya mji wa Geita


Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akipokea maandamano hayo pamoja na katibu wa wilaya ya Geita Thomas Dimme.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana waja ,wakiimba nyimbo maalum kwaajili ya siku ya mtoto wa kike.


Baadhi ya wanananchi wakifatilia kile ambacho kilikuwa kikiendelea katika maadhimisho hayo.

Kaimu Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Suzan Mashala akielezea namna ambavyo mtoto wa kike alivyo na mchango  mkubwa katika jamii .

Kwaya ya  shule ya sekondari Advetista  Mkoani Geita Wakitumbuiza katika maadhimisho ya mtoto wa kike.



Mkurugenzi wa NELICO shirika linalojihusisha na utetezi wa watoto Paulina Alex akielezea lengo la kuwepo kwa siku ya mtoto wa kike.


Wananchi wakiendelea kusikiliza na kufatilia kile ambacho kilikuwa kikiendelea katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Geita.

Wanafunzi wa shule ya msingi Kalangalala wakionesha igizo .

Onery Nery aliyevaa ngauni la kitenge na Rebeca Manase wanatoka dawati la jinsia wakielezea kesi ambazo zimekwisha kufikishwa katika dawati hilo.

Mfano wa kamba iliyowazunguka mabinti ni kati ya changamoto lukuki ambazo zinawazunguka watoto wa kike katika jamii wanazotokea.

Mkuu wa wilaya ya Geita ,Herman Kapufi akitoa hotuba mbele ya wanafunzi na wananchi waliokuwa wameuzulia katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani.

Share it:

mastaa

Post A Comment: