WATU 15 WAOKOLEWA WAKIWA HAI GEITA

Share it:
Moja kati ya wachimbaji ambaye alifukiwa na kifusi kwenye mgodi wa RZ akitoka shimoni huku akipokelewa na askali wa jeshi la zima moto

Raia wa kichina akipanda sehemu ya juu baada ya kuokolewa kwenye mgodi wa RZ

Wananchi wakishangilia kwa Furahaa baada ya zoezi la uokoaji kuwa limefanikiwa

Wananchi wakifatilia shughuli ya uokoaji.

Majeruhi wakipatiwa Huduma ya kwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga akiwashukuru wananchi kwa utulivu walionesha.

Naibu Waziri wa nishati na madini Akizungumza na wananchi wa Nyarugusu na kuwashukuru

Moja kati ya wafadhili waliojitolea kutoa huduma kwenye ajali hiyo na mkurugenzi wa Waja,Chacha Mwita akielezea namna ambavyo wameshiriki kutoa huduma

Mbunge wa CHADEMA ,Upendo Peneza akielezea namna serikali inavyotakiwa kuwajibika kuwa na vifaa vya uokoaji

Raia wa kichina akitoka eneo la Mgodini

Huduma ya kwanza ikiendelea

Naibu waziri Kalemani akiendelea kuzungumza na wananchi

Rais wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini Nchini.
Waanga wakitolewa chini ya shimo






Zoezi la uokoaji kwa wachimbaji kumi na tano (15)Kwenye mgodi wa  RZ uliopo kijiji cha Mawemeru kata ya nyarugusu limekamilika huku watu ambao walikuwa wamefukiwa wakitoka wakiwa salama baada ya kufukiwa kwa muda wa takribani siku  nne.

Zoezi hilo la uokoaji limedumu kwa muda wa siku nne(4) ambapo  lilianza tangu  January 26 majira ya saa nane usiku baada ya ofisi ya madini Mkoa  kupatiwa taarifa na kuweza kufika katika  eneo la mgodi ambao unamilikiwa na wachina lakini leseni ikiwa inaonesha umiriki kwa mchimbaji mzawa ambaye ni Bw, Ahamed Mbaraka.

Siku ya jana tarehe 28 majira ya saa moja jioni wakati wakiendelea na shughuli baadhi ya waokoaji waliweza kusikia wakigonga bomba ambalo lilikuwa likitumika kupitisha hewa na baada ya kujua wapo maeneo hayo kilichofanyika ilikuwa ni kuwapelekea Radio Koo ,ambayo ingeweza kusaidia mawasiliano lakini hata hivyo juhudi hizo hazikuweza kuzaa matunda ni kutokana na kushindwa kupatikana kwa mawasiliano.

Baada ya hatua hiyo kushindikana ilibidi waandikiwe ujumbe ambao ulitumwa kwa njia ya Bomba wakiulizwa unaendeleaje pamoja na kalamu ya kujibu ujumbe huo na walisema wapo salama na wapo kumi na tano kubwa zaidi wanaomba kupatiwa soda,biskuti pamoja na uji na kwamba wapo kumi na tano lakini mwenzao mmoja alichomwa na msumali.


Shughuli ya uokoaji imemalizika siku ya leo majira ya saa tatno ambapo baada ya kuokolewa walipatiwa huduma ya kwanza kwenye maeneo hayo ya mgodi na kisha kupelekwa Hosptary ya Mkoa kwaajili ya kufanyiwa matibabu zaidi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI DR,MEDARD KALEMANI.

Akizungumza na wananchi  baada ya kukamilika kwa zoezi zima la uokoaji Naibu waziri wa nishati na madini,Mh Medard Kalemani ameshukuru kwa wachimbaji wote kutoka salama na amempa kamishina wa madini kanda ya ziwa kufanya tasimini muda wa siku tano na shughuli ziwe zimesimama na baada ya kukamilika ndio shughuli zitaendelea.

“Lazima maeneo tunayofanyia kazi yawe salama  kwa wananchi wetu ili watu wasipoteze maisha yao eneo ambalo limetokea ajali tumelifukua fukua hivyo sio salama sana kutokana na hili nitamwacha Kamishina wa madini  hafanye shughuli ya tasimini siku tano”Alisema Kalemani.

 Katika hatua nyuingine Mh,Kalemani  amemwagiza kamishina  wa madini kumchukulia hatua mkaguzi  ambaye alitakiwa kukagua na hakukagua mgodi huo.

“Namkaguzi ambaye alitakiwa kukagua na hakukagua namwagiza kamishina wa madini kumchukulia hatua za kisheria na hatua ya pili tutapita kutambua maeneo ambayo yanamilikiwa na hayafanyiwi kazi kupatiwa wachimbaji wadogo ili waendelea na shughuli za uchimbaji”Alisisitiza Kalemani

MBUNGE WA VITI MAALUM UPENDO PENEZA
Mbunge wa viti maalum kwa Tiketi ya chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)Upendo Peneza,ameiomba serikali kuwa na utaratibu wa kuwa na vifaa vyao na kuachana na dhana ya kutegemea vifaa kutoka kwa wachimbaji wengine pindi ambapo tatizo linatokea na kuacha kutegemea kutoka kwenye mashirika mengine.

“Naomba serikali iwe na Destuli ya kuwa na vifaa vyake na kuacha kutegemea Mashirika Binafsi maana hawa watu kama GGM na  BUSWOLWA MEN,wamejitolea vifaa nadhani ni vizuri serikali ikawa na vifaa vyake na tem ambayo itasaidia kuokoa  hawa watu wamefanya kwa upendo tu kwani haikuwa ni radhima”Alisema Peneza

BAADHI YA MAJERUHI WAMEZUNGUMZIA NAMNA AMBAVYO WALIKUWA WANAISHI.

Dickson Morris,  ambaye ni mkazi wa Nzega ameelezea kuwa waliingia kwenye shimo hilo muda wa saa nane usiku na wakati wakiendelea na shughuli walisikia umeme umekata hali ambayo walijua kuwa wamekwisha kufukiwa hadi wanapata mawasiliano  hali yao ilikuwa ni mbaya zaidi.

Augustino Rabart,ameelezea kuwa yeye alikuwa chini mbili wakati anatoka kuja chini moja kwaajili ya kutoka ndipo walipokuta shimo limejifukia na kutokana na hilo ilibidi wakate tama na kujua kuwa ndio mwisho wa maisha yao lakini hata hivyo bado waliendelea na jitihada za kutaka kujiokoa na baada ya kujaribu kuchimba walikutana na dilili ambayo ilikuwa inaleta bomba kwa chini na ndipo walipoligonga na kuomba msaada.

MKUU WA MKOA WA GEITA.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga ,amewashukuru wananchi kwa utulivu walionesha pamoja na makapuni yote yaliyoshiriki kufanikisha zoezi la uokoaji.

MAKAPUNI AMBAYO YAMEFANYA ZOEZI ZIMA LA UOKOAJI

Ni kampuni ya Buswolo Min,GGM pamoja na baadhi ya wachimbaji wadogo waliopo kwenye eneo hilo wakishirikiana na Jeshi la zima Moto Mkoani Geita.

IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE


Share it:

habari

Post A Comment: