Wafanyabiashara 13 wa Wilaya za Babati na Hanang’ Mkoani Manyara, wamesalimisha katoni 1,540 za pombe zilizofungashwa kwenye karatasi (viroba) zenye thamani ya sh140 milioni.
Wafanyabiashara hao walisalimisha katoni hizo za pombe za viroba kabla ya upekuzi ulioendeshwa na polisi, maofisa wa usalama wa Taifa, chakula na dawa (TFDA) na mamlaka ya mapato nchini (TRA).
Akizungumza jana na waandishi wa habari, kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, kamishna msaidizi (ACP) Francis Massawe alisema wafanyabiashara hao walisalimisha wenyewe viroba hivyo bila kushurutishwa.
Kamanda Massawe alisema katika wilaya ya Hanang’ zilisalimishwa katoni 871 na kwa wilaya ya Babati zilisalimishwa katoni 669 na wafanyabiashara hao wanaopaswa kupongezwa kwa hatua hiyo.
Post A Comment: