MWENYEKITI WA SOKO LA CHATO AWATAKA WAFANYABIASHARA KUDUMISHA USAFI

Share it:


Mwenyekiti wa soko la Chato mjini Bw. Daudi Francisco amewataka wafanya biashara wa samaki wilayani humo kudumisha usafi katika maeneo yao ya biashara ili kuepuka magonjwa ya milipuko  yanayoweza  kujitokeza kutokana na mvua za masika zinazo endelea kunyesha.

Akizungumza na Maduka online   sokoni hapo mwenyekiti huyo amesema kuwa hali ya usafi katika eneo lake inapewa kipaumbele  hasa katika  kipindi hiki  cha mvua za masika  ambazo zinaendelea  kunyesha.

Aidha  amewataka wafanya biashara wa samaki katika maeneo yanayo zunguka ziwa victoria kufika katika soko hilo kwa lengo la kujifunza namna ya kufanya usafi na kuepuka magonjwa ya milipuko yanayo sababishwa  na uchafu.

Kwa upande wa baadhi ya wafanya biashara katika soko hilo Bi. Zuhura Benedicto na Mariam Said wamesema kuwa hali ya biashara eneo hilo imekuwa hairidhishi kutokana na serikali kuweka utaratibu wa kuuza samaki wenye ukubwa wa kuanzia sentimita 25 hadi  50 sababu inayo pelekea watu wenye kipato cha chini kushindwa kumudu gharama za kununua samaki hao.


 Sanjari na hayo wafanya biashara hao wa samaki wameiomba Serikali kupunguza vipimo  vya  ukubwa wa samaki  kwani kwa kufanya hivyo itarahisisha biashara hiyo kuwa na mzunguko  mkubwa kutokana na samaki hao kununuliwa na watu wa aina zote .

Share it:

habari

Post A Comment: