Watu watatu wakazi wa mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani na mkoani Geita wamekamatwa baada ya kukutwa katika msitu ambao umezuiwa kufanyika shughuli za kibinadamu huku wakiwa wanakata miti.
Wakizungumza watu hao ambao wametambulika kwa majina ya Paskali Songano , John Zakaria na Lukas Philipo wote wakazi wa mtaa wa mtoni katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro ambapo wamesema kuwa waliingia katika msitu huo kwa lengo la kukusanya magogo kwa ajili ya kuyatumia katika shughuli za uchomaji wa matofari .
Sanjari na hayo watu hao wamesema kuwa kabla ya kuingia katika msitu huo walipita kwa mwenyekiti wa eneo hilo na aliwaruhusu kuingia katika msitu huo kuchukua magogo ya visiki vya miti kwa kuchangia kiasi cha pesa taslimu shilingi elfu ishirini na kiongozi huyo aliwapatia stakabadhi ya halmashauli ya wilaya ya geita kama kielelezo pindi wapatapo matatizo msituni humo.
Kwa upande wake mlinzi wa msitu huo alie husika kuwakamata watu hao Bw.Zabroni Peter ameeleza kuwa amewakuta watu hao wakiwa wanakata miti kwakutumia shoka walizo kuwa nazo na siyo kwamba walikuwa wanakusanya magogo kama wanavyo eleza wao.
Aidha mwenyekiti wa mtaa huo Bw. Masunga Mbishi amekiri kuwapatia kibali cha kuwaruhusu watu hao kuingia katika msitu huo kwa lengo la kuchukua magogo na siyo kukata miti kama inavyo elezwa .
Bw. Masunga amesema watu hao waliokamatwa na mlinzi wa msitu huo hawana hatia kwasababu yeye ndiyo aliyewapatia ruhusa ya kuingia katika eneo hilo kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya miti ambayo imeharibiwa vibaya na watu wasio julikana.
Mpaka sasa watu hao wameachiwa huru.
Post A Comment: