Mwenyekiti wa chama cha Wasanii Mkoani Geita ,Bi Rose Michael(ROSE BINANZA)Akizungumza na waandishi wa habari juu ya kutokupatiwa ushirikiano na Mkuu wa Wilaya ya Geita. |
Sagari Mganga ni Moja kati ya wasanii wa maigizo akisisitiza na kuomba kupatiwa sapoti wao kama wasanii na wadau mbali mbali waliopo Wilayani na Mkoani Geita. |
Chama cha wasanii wa Maigizo Wilaya
na Mkoa wa Geita kimejitokeza hadharani na kuomba kupatiwa mchango (sapoti)
kutoka kwa wadau na viongozi Waliopo
Mkoani Humo lengo likiwa ni kutangaza kazi ambazo wanazifanya pamoja na
Kuutangaza Mkoa kwa ujumla.
Hayo yamekuja ni baada ya kuwepo kwa
taarifa ambazo wao kama chama wamedai kuwa zimewasikitisha na kuwavunja moyo
kutokana na kutokupewa ushirikiano na mkuu wa Wilaya ya Geita pindi
wanapomuhitaji kwenye kazi zao, na mwisho wa siku wameshuhudia Mkuu wa Wilaya
hiyo akiandika barua za kuunda kamati kwa ajili ya uzinduzi wa Filamu ambayo
imechezewa Mkoani humo na wasanii kutoka Zanzibar huku wao wakibakia kukosa
ushirikiano kutoka kwenye ngazi ya Wilaya.
Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii
Mkoani Humo,Rose Michael amezungumza na Maduka online na kusema kuwa kumekuwepo
na baadhi ya viongozi kutokuwapa ushirikiano, na mwisho wa siku kuwepo kwa
matabaka kwa baadhi ya wasanii wanaotoka nje ya Wilaya kupatiwa ushirikiano
wakati wao wanapowafuata kuwaomba msaada
wamekuwa wakiwakwepa.
“Mimi kama mwenyekiti wa chama cha
wasanii tumesikitishwa sana na mkuu wetu wa wilaya ya Geita kushindwa kutupatia
ushirikiano na mwisho wa siku kutoa ushirikiano huo kwa wasanii kutoka nje sisi
ndio wa kwanza kuitangaza Geita ndani na nje ya nchi leo hii kama tunahitaji
sapoti kwa viongozi wetu wa serikali wanatukwepa ni wapi tutakimbilia, nadhani
ni muhimu kwa viongozi kupenda vya kwao kwanza kabla ya vitu vya nje kama
watashindwa kutushika mkono na wakawabeba wasanii wa nje hii ni swala la ajabu sana leo hii
Wazanzibari watasaidia nini kwenye Wilaya yetu ya Geita na ndio maana
tunapoomba msaada kwenye mgodi tumekuwa tukinyimwa na kupigwa kalenda lakini wa
nje wakija wanasaidiwa kwa uharaka zaidi kiukweli imetusikitisha sana”Alisema
Rose.
Hata hivyo moja kati ya wasanii ambao
wamezindua Filamu yake inayojulikana kwa jina la WALIMWENGU,Michael Kapaya
ameelezea kuwa yeye pia ni moja kati ya watu ambao aliahidiwa na mkuu wa Wilaya
kufika kwenye shughuli yake ya uzinduzi lakini baada ya siku kuwa zimebakia
chache alimwambia kuwa hataweza kufika kutokana na kutingwa na majukumu ya
kiserikali.
“Sisi tunalia kwa ajili yake kwa sababu
ya kutokupewa sapoti na watu ambao wapo serikalini naomba watambue kuwa sanaa
ni ajira mimi namuomba mkuu wa Wilaya akae chini afikirie anatusaidiaje sisi
wasanii ambao tu katika Wilaya yake tunateseka sana mwisho wa siku huwa
tunajifikiria kukataa tamaa na hizi kazi lakini basi tu kwa sababu ndio ajira
zinazotuweka mjini”Alisema Kapaya
Maduka Online imezungumza na Mkuu wa
wilaya hiyo,Mwl Herman Kapufi ambapo ametolea maelezo malalamiko hayo na kusema
kuwa yeye hana tatizo lolote na wasanii.
“Ni
kwamba tatizo lililotokea mwaka jana kwenye shughuli ya Miss Geita
walikuja kuniomba kuwa niwasaidie kupata ufadhili kutoka Mgodi wa dhaahabu wa
Geita (GGM) na mimi niliwaombea na
walifanikisha kupatiwa shilingi milioni Kumi (10) lakini fedha hizo ambazo
waliomba zilileta ugomvi na kushindwa kufanya lengo ambalo lilikusudiwa hali
hiyo ilipelekea kunivunja moyo maana
kama kwa jambo dogo wameshindwa kuwa waaminifu sidhani kama wanaweza kuwa
waaminifu kwa mambo makubwa”Alisema Mh,Kapufi.
Kuhusu swala la kuwasaidia wasanii wa
nje ya Wilaya ya Geita na kutokuwapatia msaada wao wa ndani Mkuu wa Wilaya
amesema kuwa msaada wa GGM umetoka kwa
Bw ,Shayo yeye amefanya kazi ya kusambaza barua ni kutokana na kuombwa na
Waziri wa Zanzibar wa michezo kupitia kwa aliyekuwa waziri wa sekta hiyo
Mh,Nape Nnauye kuwapa msaada wa kupata wafadhili ambao watawasaidia kwenye
uzinduzi wao.
Mh,Kapufi ameongeza kwa kuwashauri
wasanii kuwa na umoja kutokana na kuwapo makundi ambayo yamekuwa yakiwagawa
kwenye shughuli zao za sanaa huku akiwasisitiza kuwa na akauti pamoja na ofisi
ambazo zitawasaidia kuwatambulisha.
IMEANDALIWA NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLINE .
Post A Comment: