WANAFUNZI WAJENGEWE MAADILI NA UZALENDO KWA TAIFA

Share it:
Frederick Joseph Ndahani Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, wakati akizunguza na hadhara ya wananchi
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ,Amour Hamad Amour akiweka Jiwel la Msingi kwenye Mabweni ya shule ya Sekondari ya Nyachiluluma
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ,Amour Hamad Amour,akikagua Bweni la wasichana la shule ya Sekondari Nyachiluluma



Wazazi,Walimu na Jamii imetakiwa kuwajengea Watoto pamoja na wanafunzi ambao wapo shule za Msingi na Sekondari misingi ya maadili na uzalendo katika ufundishaji wa Masomo na malezi pindi wanapokuwa Nyumbani  ili kuweza kuwasaidia kuwa na moyo wa kulipenda Taifa na  kulinda  rasilimali zilizopo Nchini.



Rai hiyo imetolewa na  Frederick Joseph Ndahani Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, wakati akizunguza na hadhara ya wananchi, wanafunzi pamoja  na walimu wa sekondari ya Busanda iliyopo Kata ya Busanda katika  Halmashauri ya Wilaya ya Geita.


Ndahani, amesema kama wanafunzi watajengwa katika Misingi iliyo imara hapo badae, watakuwa viongozi  bora wenye kusimamia ukweli katika shughuli za ujenzi wa taifa.

“Tunatambua kwamba watoto hawa wakijengewa msingi imara ndio wanaweza kuja kuwa mabarozi wazuri wa kupinga vitendo vya rushwa ambavyo vimekuwa vikiathiri kwa kiasi kikubwa pato la Taifa na kuwanyima watu haki “Alisisitiza Ndahani

Awali akizindua Bweni la wanafunzi wa kike  katika Sekondari ya Nyachiluluma lililogharimu fedha za Wananchi, halmashauri na serikali kuu zaidi ya Sh. Milioni 130, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Amour Hamad Amour amewasisitiza wanafunzi wa kike kutumia nafasi hiyo ambayo serikali imeona ni vyema kuweka mabweni kwa kusoma kwa bidii na kuachana na mambo ambayo yanaweza kuwasababisha kutokutimiza malengo yao.


Kwa Upande wake  Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyachiluluma Richard Musiba amesema mwaka wa jana Wanafuzi watatu walibainika kuwa na ujauzito na mwaka huu ni wanafunzi wawili  na wote  wamekwisha ondolewa shuleni.


Share it:

habari

Post A Comment: